Yanga mazoezini Uturuki jana |
Na Baraka Kizuguto,
Antalya
KLABU ya Yanga
ya Dar es Salaam, kesho itashuka dimbani kucheza mchezo wa kirafiki na Arminia
Bielefeld ya Ujerumani, mchezo utakaofanyika katika mji wa Antalya, Uturuki.
Yanga ambayo
imeweka kambi ya mafunzo mjini Antalya, itatumia mchezo huo kama fursa pekee ya
kuweza kujipima uwezo dhidi ya timu hiyo ya Ujerumani ambayo pia imekuja kuweka
kambi ya mafunzo kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Daraja la Pili
Ujerumani.
Kocha Mkuu
wa Yanga, Mholanzi Ernest Brandts amesema kwao ni furaha kwa kupata nafasi ya
kucheza na timu kubwa kama ya Armini Bielefeld ambayo ina wachezaji wa kiwango
cha kimataifa, hivyo anaamini utakua ni mchezo safi na kuwavutia.
“Unajua tuna
siku sita tangu tufike hapa (Antalya Uturuki) na tumeshafanya mazoezi kwa siku
nne, hivyo fursa ya kupata mchezo wa kirafiki ni nzuri sana kwetu kwani itanipa
nafasi ya kuona wachezaji wangu wameshayashika kwa kiasi gani mafunzo yangu,”
alisema Brandts.
Arminia
Bielefeld imeshawasili mjini Antalya kwa
ajili ya kambi yake ya mafunzo na hivyo kwao pia ni fursa nzuri ya kuweza
kujipima uwezo na timu ya Yanga ambao ni mabingwa mara 23 Tanzania Bara.
Jana asubuhi
Yanga imeendelea na mazoezi katika viwanja wa Fame Residecne tayari kabisa
kujiandaa na mchezo huo.
Kikosi cha
wachezaji 27 waliopo mjini Antalya wote wako katika hali nzuri na hakuna majeruhi
hata mmoja hali itakayompa kocha Brandts kuamua kumtumia mchezaji yoyote katika
mchezo huo.