Jamal Malinzi |
KAMATI ya
Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imesema waliowekewa pingamizi na
wa walioweka pingamizi hawaruhusiwi kufika katika kikao cha kesho (Januari 30
mwaka huu) wakiwa na vikundi vya ushangiliaji au wapambe.
Kikao cha
kupitia pingamizi kitafanyika saa 4 asubuhi na wapambe au washabiki wa waombaji
uongozi pamoja na waweka pingamizi hawakiwi kuwepo kwenye eneo la kikao hicho.
Wote
walioweka pingamizi na waliowekewa pingamizi barua zao za mwito wa kuhudhuria
kikao cha Kamati ya Uchaguzi ya TFF
zimeshatumwa kwenye anwani za barua-pepe zilizo kwenye taarifa za pingamizi au
kwenye fomu za maombi ya uongozi.
Leo waombaji
uongozi watatumiwa barua za mwito kwa barua-pepe wa kuhudhuria usaili
utakaofanyika tarehe 01-02 Februari 2013. Tarehe 01 Februari 2013 watasailiwa
waombaji uongozi wa TPL Board na waombaji ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF
kupitia Kanda ya 1 hadi Kanda ya 8. Waombaji uongozi kupitia Kanda ya 9 hadi ya
13 na waombaji uongozi wa Makamu wa Rais na Rais wa TFF watasailiwa tarehe 02
Februari 2013 kuanzia saa 4 asubuhi.
Vyombo vingi
vya habari vimeonyesha nia ya kuwepo mdahalo wa wagombea uongozi katika TPL
Board na TFF. Kanuni za Uchaguzi za TFF hazizuii jambo hilo kufanyika, bali tu
lizingatie Kanuni za Uchaguzi za TFF. Mojawapo ya mambo ya kuzingatiwa ni
kwamba mdahalo huo ufanyike wakati wa kipindi cha Kampeni na usiwe na taswira
ya kuwapendelea au kuwabagua baadhi ya wagombea. Kanuni hazimlazimishi mgombea
kushiriki mdahalo.
Pia ni vema
mdahalo ukaandaliwa na kuratibiwa na
Taasisi inayounganisha vyombo vya habari au waandishi wa habari kama TASWA.
Kamati ya Uchaguzi ya TFF lazima ijulishwe kwa maandishi nia hiyo ya kufanyika
mdahalo na utaratibu utakaotumika mapema kabla ya kufanyika mdahalo huo ili kujiridhisha
kuwa utaratibu utakaotumika kuandaa na kuendesha mdahalo haukiuki kanuni za
Uchaguzi za TFF.
Kamati ya
Uchaguzi ya TFF inavishukuru vyombo vya habari kwa kuzingatia Kanuni za
Uchaguzi hadi sasa na kuwaomba waendelee kufanya hivyo hadi mwisho wa mchakato
wa uchaguzi.