![]() |
Manji akizungumza na Waandishi leo baada ya kuchukua fomu |
Na Boniface Wambura
WADAU watatu
wa soka nchini, leo mchana wamechukua fomu za kuwania urais wa Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF) na kufanya idadi ya waliojitokeza hadi sasa katika uchaguzi huo
utakaofanyika Februari 24 mwaka huu kufikia 30.
Hata hivyo,
idadi hiyo ni kwa wale wanaochukua fomu hizo katika ofisi za TFF, kwani
vilevile zinapatikana kupitia tovuti ya TFF ya www.tff.or.tz ambapo mwisho wa
kuchukua na kurejesha ni saa 10 kamili alasiri Januari 18 mwaka huu.
Waliochukua
leo (Januari 16 mwaka huu) kuwania urais ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa TFF,
Athuman Jumanne Nyamlani, Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Kagera
(KRFA), Jamal Emil Malinzi na Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa
Kigoma, Omari Mussa Nkwarulo.
Mwengine
aliyechukua leo ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mbeya
(MREFA), Elias Mwanjala anayewania ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF
kuwakilisha Kanda ya Iringa na Mbeya.
Orodha
kamili ya wadau waliochukua fomu kwenye ofisi za TFF ni Athuman Jumanne
Nyamlani, Jamal Emil Malinzi na Omari Mussa Nkwarulo (urais), Michael Wambura,
Ramadhan Nassib na Wallace Karia (umakamu wa rais).
Kwa upande
wa wajumbe wa Kamati ya Utendaji na kanda zao kwenye mabano ni Salum Chama
(Kagera na Geita), Mugisha Galibona, Samuel Nyalla, Titus Osoro na Vedastus
Lufano (Mara na Mwanza).
Epaphra Swai
na Mbasha Matutu (Shinyanga na Simiyu), Charles Mugondo na Elly Mbise (Arusha
na Manyara), Yusuph Kitumbo (Kigoma na Tabora), Ayubu Nyaulingo, Nazarius Kilungeja
na Selemani Kameya (Katavi na Rukwa) na James Mhagama (Njombe na Ruvuma).
Athuman
Kambi (Lindi na Mtwara), Hussein Mwamba na Stewart Masima (Dodoma na Singida),
Farid Nahdi na Twahili Njoki (Morogoro na Pwani), Elias Mwanjala (Iringa na
Mbeya), Khalid Mohamed (Kilimanjaro na Tanga) na Muhsin Balhabou, Shaffih Dauda
na Zafarani Damoder (Dar es Salaam).
Kwa upande
wa Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board) waliochukua fomu kwenye ofisi za TFF mpaka sasa
ni wawili tu. Yusuf Manji amechukua fomu ya uenyekiti wakati Said Mohamed
amechukua fomu ya kuwania umakamu mwenyekiti.