Viongozi wa Simba, Yanga na TFF wakiwa na Kavishe |
Mwalusako kulia akitoa shukrani zake kwa wadhamini, katikati ni Ofisa wa TFF, Saad Kawemba na kushoto kabisa ni Kavishe |
Kawemba katikati akitoa nasaha zake |
Kamwaga kushoto akitoa shukrani kwa wadhamini |
Na Prince Akbar
IKIWA ni
sehemu ya udhamini wake, bia ya Kilimanjaro Premium Lager imekabidhi vifaa vya
michezo kwa klabu maarufu za Simba SC na Young Africans SC kwa ajili ya awamu
ya pili ya msimu wa 2012/13 wa Ligi Kuu inayotarajiwa kuanza mwishoni mwa wiki
hii.
Meneja wa
bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe alisema “Bila shaka Simba na
Yanga ndio klabu kubwa zaidi hapa Tanzania zikiwa kwa pamoja zimeweza kupata
mafanikio makubwa kwa kipindi kirefu na bado zinaendelea kufanya vizuri.
Tunajivunia kuweza kuziunga mkono klabu hizi katika jitihada za kuwania taji la ligi kuu msimu huu.
Vifaa
ambavyo leo tunatoa ni pamoja na mipira, viatu, soksi, shin guards, nguo za
mazoezi, nguo za kawaida, gloves na vitu vingine vingi ambavyo vitawezesha timu
hizi za Simba na Yanga kucheza wakifurahia kuvaa vifaa vyenye ubora wa hali ya
juu.
Kilimanjaro
Premium Lager kama mdhamini mkuu wa Simba na Yanga, na kinywaji kinachoongoza
katika udhamini wa soka hapa nchini tunadhani kwamba uhusiano wetu na klabu
hizi ni kiungo muhimu sana katika kuendeleza mpira wa miguu hapa Tanzania.
Tutaendelea kutimiza majukumu yetu kwa klabu hizi na kama ilvyo kawaida yetu,
tutahakikisha tunalifikisha soka la Tanzania kwenye kilele cha mafanikio. kabisa kwani, pamoja na uhusiano huo mzuri na
klabu hizi mafanikio makubwa yanatarajiwa katika kuendeleza soka la Tanzania.
Kavishe
alisema kuwa ushirikiano kati ya Kilimanjaro Premium Lager na klabu hizo
umesimamia katika misingi ya kufanya kazi pamoja, uadilifu na kuendelea kupata
mafanikio. “Ushirikiano huu unasaidia kukuza mpira wa Tanzania, kuleta
msisimko, na kuvutia mashabiki wengi wa mpira wakati na vilevile kuwaweka
wachezaji wa Tanzania katika nafasi nzuri ya kimataifa.
Tunachukua
nafasi hii kuwashukuru viongozi wa Simba na Yanga walioko hapa, mashabiki wote,
vyombo vya habari na wadau wote wa mpira kwa ushirikiano mzuri tunaoendelea
kupata kwenye udhamini wetu na hiyo ndio siri ya mafanikio ya uhusiano wetu na
klabu hizi mbili maarufu.
“Tunaahidi ushirikiano kwa klabu hizi nzuri na
kama tunavyosema kila mara lengo letu ni kufikisha mpira wa Tanzania kwenye
ngazi za kimataifa na kuwafikisha mashabiki wa mpira na wapenzi wa Kilimanjaro
Premium Lager kwenye kilele cha mafanikio.”