Selemba katika mechi ya jana, cheki kitu alichomfanya Khamis Mcha 'Vialli' |
Na Mahmoud Zubeiry,
Zanzibar
KOCHA wa
Azam FC ya Dar es Salaam, Muingereza Stewart Hall amesifia kiwango cha kiungo
wa zamani wa timu yake, Suleiman Kassim ‘Selembe’ ambaye kwa sasa anachezea
Coastal Union ya Tanga kwamba kimepanda.
Pamoja na
kusifia kiwango cha mchezaji huyo, Hall amesema kiungo hana nafasi Azam, kwa
kuwa sasa ina wachezaji bora zaidi yake kama Kipre Herman Tchetche kutoka Ivory
Coast na Brian Umony kutoka Uganda.
“Kweli
ameimarika tofauti na alivyokuwa Azam, lakini sijutii kwa sababu kikosini nina
wachezaji wazuri kama Kipre Tchetche na Umony, nitamkumbuka Selembe?”alisema.
Azam FC na
Coastal Union jana zilitoshana nguvu baada ya kutoka sare ya bila kufungana katika
mchezo wa Kundi B, Kombe la Mapinduzi usiku huu kwenye Uwanja wa Amaan,
visiwani hapa.
Coastal leo
ndio waliotawala mchezo na kupoteza nafasi kama tatu za wazi za kufunga mabao,
kutokana na umakini mdogo kila walipopata nafasi hizo.
Azam
walipata nafasi moja nzuri kipindi cha pili, lakini walinzi wa Coastal
walisimama imara na kuondosha kwenye hatari jaribio hilo.
Katika
mchezo huo, kikosi cha Azam FC kilikuwa; Mwadini Ally, Himid Mao, Samir Hajji
Nuhu, David Mwantika, Joackins Atudo, Kipre Balou, Salum Abubakar, Humphrey
Mieno, Gaudence Mwaikimba, Kipre Tchetche/Brian Umony dk 24 na Hamisi Mcha
‘Vialli’/Seif Abdallah dk 66.
Coastal
Union; Juma Mpongo, Ismail Khamis, Othman Tamim, Philip Metusela, Mbwana Khamis
‘Kibacha’, Hamisi Shengo, Suleiman Kassim ‘Selembe’/Hussein Twaha dk 50, Jerry
Santo, Mohamed Mtindi, Soud Othman/Razack Khalfan dk90 na Danny Lyanga/Joseph
Mahundi dk 90.
Katika
mchezo wa kwanza wa kundi hilo, Miembeni iliitandika mabao 4-1 Mtibwa Sugar
kwenye Uwanja wa mao Dze Tung.
Mabao ya
Miembeni yalitiwa kimiani Adeyum Saleh Ahmed dakika ya 41 na 72, Mohamed
Hamdani na Rashid Roshwa dakiaka ya 74, wakati la Mtibwa la kufutia machozi
lilifungwa na Juma Mpakala dakika ya 10.