Okwi |
Na Mahmoud Zubeiry
PAMOJA na kumuuza kwa dau la dola za Kimarekani, 300,000 mshambuliaji
wake wa kimataifa wa Uganda, Emannuel Okwi katika klabu ya Etoile du Sahel ya
Tunisia, lakini klabu hiyo inaweza kujikuta inaambulia dola 200,000 tu.
Hiyo inatokana na makato mengine ya kisheria yanayoingia
katika mauzo hayo, ikiwemo asilimia 20 ya klabu yake ya zamani, SC Villa ya Uganda,
ambayo ni sawa na dola 60,000.
Pamoja na hayo, inaelezwa kuna fungu la wakala aliyefanikisha
mpango huyo ambaye ana mkataba na Okwi.
Simba ilimuuza Okwi klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia kwa dau
la dola za Kimarekani 300,000, zaidi ya Sh Milioni 450 za Tanzania.
Okwi, aliyezaliwa Desemba 25, mwaka 1992 aliisajiliwa Simba
akitoea SC Villa ya Uganda mwaka 2010 akiwa kinda wa miaka 17, akisajiliwa kwa
dau la dola za Kimarekani 40,000.
Baada ya kumaliza mkataba wake wa awali, Desemba mwaka jana aliongeza
mkataba wa miaka miwili na Simba SC ambao kabla hajaanza kuutumikia, anahamia
Sahel.