Na Mahmoud Zubeiry,
Zanzibar
NAHODHA wa
Tusker, Joseph Shikokoti amesema kwamba haoni timu ya kuwazuia kutwaa Kombe la Mapinduzi,
michuano inayoendelea visiwani hapa.
Akizungumza jana,
Shikokoti aliyewahi kuchezea Yanga alisema kwamba anafahamu Simba na Azam ni
wazuri na anajua mojawapo watakutana nayo fainali, lakini amesistiza hakuna
kati yao inayoweza kuwazuia wasitwae Kombe.
“Hili Kombe
letu, tumeona uwezo wa timu zote, hata Simba na Azam ni wazuri, lakini
tutawafunga wote tukikutana nao, hawana uwezo wa kutuzuia,”alisema Shikokoti.
Tusker, mabingwa
wa Kenya, jana jioni walikuwa timu ya kwanza kufuzu Nusu Fainali ya Kombe la
Mapinduzi, baada ya kuilaza Jamhuri ya Pemba bao 1-0, lililofungwa na
mshambuliaji wake hatari, Jesse Were dakika ya 23 kwenye Uwanja wa Amaan,
Zanzibar. Ushindi huo, umewafanya wababe hao wa soka ya Kenya wamalize mechi
zao za Kundi A wakiwa na pointi saba, wakifuatiwa na Simba SC iliyomaliza na pointi
tano.
Jamhuri iliyomaliza
na pointi tatu na Bandari ambayo imeambulia pointi moja, zimeaga mashindano
haya. Simba na Tusker zinasubiri mechi za leo za mwisho za Kundi B ili kujua
wapinzani wao katika Nusu Fainali.