Kuna pingamizi lolote dhidi ya Malinzi, mgmbea urais? |
Na Prince Akbar
BAADA ya
kupitia fomu za waombaji uongozi Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Kamati ya
Uchaguzi ya shirikisho hilo leo inaanza mchakato wa pingamizi dhidi ya
wagombea.
Ofisa Habari
wa TFF, Boniface Wambura Mgoyo amesema kwamba, leo saa 10:00 jioni Kamati ya
Uchaguzi itabandika kwenye ubao wa matangazo wa TFF majina ya waombaji ili
kutoa fursa kwa kipindi cha pingamizi.
Wambura amesema
mwisho wa kupokea pingamizi dhidi ya waombaji uongozi ni Januari 26, mwajka huu
saa 10:00 jioni.
Jumla ya
watu 50 kati ya 52 waliochukua fomu kuomba kuwania nafasi mbalimbali za uongozi
katika uchaguzi wa TFF utakaofanyika Februari 24, mwaka huu wamerejesha fomu
hizo.
Waombaji
ambao hawakurejesha fomu ni Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ aliyekuwa akiomba ujumbe
wa Kamati ya Utendaji kuwakilisha mikoa ya Morogoro na Pwani, na Shufaa Jumanne
aliyekuwa akiomba kuwakilisha Kanda ya Dar es Salaam.
Orodha
kamili ya wagombea waliorejesha fomu ni Athumani Nyamlani, Jamal Malinzi, Omari
Nkwarulo na Richard Rukambura wanaogombea Urais, nafasi inayoachwa wazi na
Leodegar Tenga anayeng’atuka, Michael Wambura, Ramadhani Nassib na Wallace
Karia wanaogombea Makamu wa Rais, nafasi inayoachwa wazi na Nyamlani,
anayehamia kwenye Urais.
Kwa upande
wa ujumbe wa Kamati ya Utendaji ni Abdallah Musa, Salum Chama na Kaliro Samson
(Kagera na Geita), Jumbe Magati, Mugisha Galibona, Richard Rukambura, Samuel
Nyalla, Titus Osoro na Vedastus Lufano (Mara na Mwanza).
Epaphra Swai
na Mbasha Matutu (Shinyanga na Simiyu), Charles Mugondo, Elly Mbise na Omari
Walii (Arusha na Manyara), Ahmed Mgoyi na Yusuph Kitumbo (Kigoma na Tabora),
Ayubu Nyaulingo, Blassy Kiondo, Nazarius Kilungeja na Selemani Kameya (Katavi
na Rukwa) na James Mhagama na Stanley Lugenge (Njombe na Ruvuma).
Athuman
Kambi, Francis Ndulane na Zafarani Damoder (Lindi na Mtwara), Hussein Mwamba na
Stewart Masima (Dodoma na Singida), Farid Nahdi, Hassan Othman Hassanoo, Riziki
Majala na Twahili Njoki (Morogoro na Pwani), David Lugenge, Elias Mwanjala,
Eliud Mvella na John Kiteve (Iringa na Mbeya), Davis Mosha, Khalid Mohamed na
Kusiaga Kiata (Kilimanjaro na Tanga) na Alex Kamuzelya, Juma Pinto, Muhsin
Balhabou, Omari Abdulkadir na Shaffih Dauda (Dar es Salaam).
Aidha, waombaji
wote sita wa uongozi katika Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board) ambayo uchaguzi wake
utafanyika Februari 22 mwaka huu wamerejesha fomu.
Kwa upande
wa Mwenyekiti waombaji ni Hamad Yahya wa Kagera Sugar na Yusuph Manji wa Yanga
wakati Makamu Mwenyekiti aliyeomba ni Said Mohamed wa Azam.
Nafasi mbili
za ujumbe wa Bodi ya Ligi Kuu kwa klabu za Daraja la Kwanza zimeombwa na watu
watatu. Waombaji hao ni Christopher Peter Lunkonde wa Moro United, Kazimoto
Miraji Muzo wa Pamba ya Mwanza na Omari Khatibu Mwindadi.