Simba SC |
Na Mahmoud Zubeiry,
Zanzibar
SIMBA SC
inashuka dimbani kwenye Uwanja wa Amaan visiwani hapa kuanzia saa 2:00 usiku wa
leo, kumenyana na Tusker ya Kenya katika mchezo wa Kundi A, Kombe la Mapinduzi.
Mchezo huo,
utatanguliwa na mchezo mwingine wa kundi hilo, kati ya Jamhuri na Bandari
kwenye Uwanja wa Mao Dze Tung kuanzia saa 10:30.
Kocha
Msaidizi wa Simba SC, Jamhuri Mussa Kihwelo ‘Julio’ amesema kwamba mabingwa hao
wa Kenya watarajie shughuli tofauti kutoka kwa mabingwa wa Bara leo, tofauti na
ilivyokuwa timu hizo zilipokutana wiki iliyopita Dar es Salaam na Tusker wakashinda
3-0.
“Tusker
wajue Dar es Salaam hawakuifunga Simba, walikafunga ka Simba, sasa ndio
wanacheza na Simba na watake wasitake wataumia,”alisema Julio.
Kocha mpya
wa Simba SC ya Dar es Salaam, Mfaransa Patrick Liewig aliyerufahishiwa na uwezo
wa wachezaji wa timu hiyo baada ya kuwashuhudia juzi wakiwachapa mabingwa wa
Zanzibar, Jamhuri ya Pemba mabao 4-2 kwenye Uwanja huo huo wa Amaan mjini hapa,
jana alianza kazi rasmi.
Mfaransa
huyo aliyetua Dar es Salaam Jumatatu kabla ya Jumanne kusaini mkataba wa miezi
18 wa kuifundisha timu hiyo na kuja Zanzibar juzi kuungana na timu, leo anaweza
kukaa kwenye benchi pamoja na wasaidizi wake, Julio na Mganda, Moses Basena.
Liewig ni
kocha wa zamani wa Akademi ya Paris Saint Germain (PSG) ya Ufaransa, ASEC
Mimosas ya Ivory Coast na Club Africain ya Tunisia, ambaye ana Stashahada ya
Juu ya ukocha na Shahada ya tatu ya ualimu wa soka ya vijana aliyotunukiwa na
Mkurugenzi wa Ufundi wa Ufaransa, Gerard Houiller, anatarajiwa kwenda Zanzibar
kesho.
Liewig pia
amehudhuria kozi za ufundishaji mazoezi ya viungo Juni mwaka 1999 katika Chuo
Kikuu cha Dijon.
Kwa upande
wa uzoefu, Liewig alifanya kazi PSG kuanzia mwaka 1989 hadi 1999 kama Kocha
Mkuu wa akademi na kuna wakati alikuwa akishirikishwa pia katika programu za
timu A, ingawa majukumu yake zaidi yalikuwa ni kwa Under 20, Under 18 aliowawezesha
kutwaa Kombe la French Junior Gambardella na Under 16.
Kuanzia
mwaka 1989 hadi 1990: alikuwa Meneja
Mkuu wa Tomislav IVIC, 1990 hadi 1991 alikuwa Msaidizi wa Henri Michel, 1991 hadi
1994 alikuwa Msaidizi wa Artur Jorge, 1994 hadi 1996 alikuwa Msaidizi wa Luis Fernandez,
1996 hadi 1998: alikuwa Msaidizi wa Ricardo Gomez, 1998 hadi 1999 alikuwa
Msaidizi wa Alain Giresse.
Liewig pia
alifundisha Al Wahda FC ya Abu Dhabi kuanzia 1999 hadi 2001, ambayo aliipa
ubingwa wa Ligi Kuu ya nchi hiyo na Kombe la Ligi.
Januari
mwaka 2003 alikuwa Msimamizi wa Chama cha Soka UAE katika fainali za Afrika za
U20 nchini Burkina Faso.
Kuanzia
mwaka 2004 hadi 2009 alikuwa Kocha wa ASEC Mimosas ya Ivory Coast aliyoipa
mataji matatu ya Ligi Kuu ya nchini humo mfululizo, 2004, 2005 na 2006, Super
Cup ya nchini humo 2005, 2007, 2008 na 2009 na akaiwezesha kufuzu hatua ya
makundi ya Ligi ya Mabingwa mara tatu, mara moja akiifikisha Nusu Fainali.
Amekuwa
Kocha bora wa Ivory Coast miaka mitatu mfululizo, 2004, 2005 na 2006 na tangu Septemba
mwaka jana hadi Juni mwaka huu, alikuwa kocha wa Club Africain ya Tunisia
WAFUNGAJI WA MABAO:
Jesse Were Tusker FC 2
Adeyum Saleh
Miembeni 2
Mfanyeje
Mussa Jamhuri 2
Ismail Dunga
Tusker FC 1
Michael
Olunga Tusker FC 1
Andrew
Tolowa Tusker FC 1
Amour Janja Bandari 1
Mohamed
Hamdani Miembeni 1
Rashid Roshwa Miembeni 1
Juma Mpakala
Mtibwa 1
Felix Sunzu Simba SC 1
Shomary
Kapombe Simba SC 1