Na Mahmoud Zubeiry,
Zanzibar
SIMBA SC
itamenyana na Azam FC katika Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi Januari 10,
mwaka huu kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Hiyo inafuatia
Azam kutoka sare ya bila kufungana na Mtibwa Sugar usiku huu kwenye Uwanja wa
Amaan visiwani hapa, katika mchezo wa mwisho wa Kundi B la michuano hiyo.
Azam imemaliza
na pointi tano na kuongoza Kundi B, ikifuatiwa na Miembeni iliyomaliza na
pointi nne.
Miembeni itamenyana
na kinara wa Kundi A, Tusker ya Kenya keshokutwa katika Nusu Fainali ya kwanza.
Katika mchezo
wa leo, Azam ikiongozwa na washambuliaji wawili, Gaudence Mwaikimba aliyekuwa
katikati na Brian Umony aliyekuwa akishambulia kutokea pembeni ililitia
misukoko miwili mitatu lango la Mtibwa, lakini leo kipa Hussein Sharrif
‘Casillas’ alisimama imara kwa dakika zote 90 na kuokoa hatari zote.
Mtibwa
iliyocheza na washambuliaji wawili pia, Hussein Javu na Juma Zuilio ililitia
misukosuko pia lango la Azam, lakini Mwadini Ally kipa wa Azam alikuwa makini
kuokoa hatari zote.
Azam FC;
Mwadini Ally, Himid Mao, Samih Haji Nuhu, David Mwantika, Jockins Atudo,
Michael Bolou, Brian Umony/Seif Abdallah dk70, Salum Aboubakar, Gaudence
Mwaikimba, Humphrey Mieno na Khamis Mcha
‘Vialli’/Uhuru Suleiman dk47.
Mtibwa
Sugar;Hussein Sharif, Khamis Issa, Yusuf Nguya, Rajab Mohamed, Salvatory Ntebe,
Babu Ally Seif, Vincent Barnabas, Rashid Gumbo, Hussein Javu, Juma Zuilio na
Ally Mohamed.