EMMANUEL Okwi na Mrisho Ngassa 'Anko' wameipotezea Simba nafasi ya kujipima na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Simba walipangiwa kucheza na Congo waliopiga kambi hapa kujiandaa na fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, mwaka huu. Mechi hiyo ilitakiwa kuchezwa leo Jumamosi. Kocha wa Simba, Patrick Liewig alifuta mchezo huo kutokana na kuwa na wachezaji wachache. Okwi anayeingarisha simba kutokana na kiwango chake, tangu alipokwenda kwao kwa mapumziko na kucheza mashindano ya Chalenji hajaripoti kambini na sasa imeripotiwa yupo Tunisia akifanya majaribio na klabu ya Esperance. Ngassa pamoja na Amir Maftah, Juma Kaseja, Amri Kiemba, Mwinyi Kazimoto na Shomari Kapombe wako na Taifa Stars huko Ethiopia. Kocha wa zamani wa Simba, Talib Hilal, ambaye ni mwenyeji wao hapa, alisema Congo, ambayo inaongozwa na nahodha wake, Tresor Mputu walitaka mechi hiyo leo Jumamosi. Hata hivyo, Simba ina wachezaji wanane tu hapa; Felix Sunzu, Abel Dhaira, Nassor Said 'Cholo', Haruna Shamte, Kigi Makassy, Salim Kinje, Haruna Moshi 'Boban' na Ramadhani Chombo 'Redondo'. Wachezaji wengine walibaki Zanzibar kwenye mashindano ya Kombe la Mapinduzi kabla ya kuondolewa hatua ya nusu fainali na Azam FC. Simba watacheza mechi ya kwanza dhidi ya timu ya Olimpiki ya Oman, Jumanne ijayo. Watajipima ubavu na Suwqi Januari 18 na watamaliza na Fanja FC. |
Man United eye Matheus Cunha but must sell before being able to afford
Wolves' asking price for 15-goal star
-
Manchester United are on a long list of Premier League clubs who are
interested in signing 25-year-old Brazilian forward Matheus Cunha from
Wolves this sum...
47 minutes ago