Shomary Kapombe kulia, moja ya vipaji vilvyoibuliwa Morogoro |
Na Daud Julian,
Morogoro
KLABU za
soka ya vijana, watoto na wanawake katika Manispaa ya Morogoro vimeanzisha
umoja wao kwa lengo la kujipatia mafanikio zaidi katika mchezo huo.
Uamuzi wa
kuunda umoja huo ulifikiwa wikiendi iliyopita katika mkutano wa viongozi wa
vilabu hivyo uliofanyika katika ukumbi wa DDC, mjini hapa.
Viongozi wa
muda waliochaguliwa kuongoza umoja huo na nafasi zao zikiwa katika mabano ni
Tike Tike Dimoso (mwenyekiti), Patrick Fulano (makamu mwenyekiti), Gasper
Mashenene (katibu mkuu), Adam Costantino (mweka hazina), Daudi Julian (mratibu)
na Juma Mgonja (mjumbe).
Akizungumza
mara baada ya uchaguzi huo, mwenyekiti wa Umoja huo, Dimoso alisema lengo ni
kuhakikisha vilabu vya soka ya vijana, watoto na wanawake katika manispaa ya
Morogoro vinapiga hatua kubwa katika mchezo huo na hivyo kujiweka katika
mazingira mazuri ya kuibua vipaji zaidi vya wanasoka chipukizi.
Dimoso
alisema uongozi wa Umoja huo tayari umeshaanza kutekeleza majukumu yake ikiwa
ni pamoja na kuandaa rasimu ya katiba.
“Huu ni
umoja wa aina yake na ni wa kwanza kuanzishwa katika manispaa ya Morogoro na
mkoa kiujumla hivyo naamini tutafanikiwa”, alisema.
Mwenyekiti
huyo ametoa wito kwa wadau wa soka mkoani Morogoro kuusaidia Umoja huo kwa hali
na mali ili kuhakikisha unatimiza malengo yake.
Vilabu
vilivyokutana na kuasisi Umoja huo ni Al Futuh United, Young Boys, Jamhuri
Boys, CIDA Kids, Mazimbu FC, Mwere Kids, New Kids na Kingo Kids.