// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MCHAKATO TIKETI ZA ELEKTRONIKI WAFIKIA ASILIMIA 80 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MCHAKATO TIKETI ZA ELEKTRONIKI WAFIKIA ASILIMIA 80 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, January 20, 2013

    MCHAKATO TIKETI ZA ELEKTRONIKI WAFIKIA ASILIMIA 80


    Mashabiki Uwanja wa Taifa 

    Na Boniface Wambura
    UJENZI wa vifaa (turnstiles) vitakavyotumika kwa ajili ya tiketi za elektroniki kwenye viwanja saba kati ya nane vitakavyotumia mfumo huo umekamilika kwa asilimia 80.
    Viwanja hivyo ni Chamazi (Dar es Salaam), Jamhuri (Morogoro), Kaitaba (Bukoba), Sokoine (Mbeya), Sheikh Kaluta Amri Abeid (Arusha), na Mkwakwani (Tanga).
    Wakati Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam tayari una turnstiles, Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza bado haujaruhusu ufungaji wa vifaa ukisubiri idhini kutoka kwa wamiliki wake (CCM Makao Makuu).
    Vifaa vitakavyotumika kusoma tiketi za elektroniki katika viwanja hivyo vinatarajiwa kuwa vimefungwa kufikia Februari 20 mwaka huu.
    Hakutakuwa na matumizi ya fedha taslimu mara baada ya mradi huo wa tiketi la elektroniki kuanza, kwani tiketi zitakuwa zikinunuliwa kwa kadi maalumu (smart card) katika vituo mbalimbali vitakavyotangazwa baadaye.
    Benki ya CRDB ndiyo iliyoingia mkataba na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kutengeneza tiketi za elektroniki baada ya kuibuka mshindi kwenye tenda.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: MCHAKATO TIKETI ZA ELEKTRONIKI WAFIKIA ASILIMIA 80 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top