Lulu |
Na Happiness Katabazi
LICHA ya Mahakama
Kuu Kanda ya Dar es Salaam kumpa dhamana msanii wa Filamu nchini, Elizabeth
Michael ‘Lulu’, anayekabiliwa na kesi ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa msanii
mwenzake, Steven Kanumba lakini amerudishwa rumande baada ya Msajili wa
Mahakama kukosekana kukamilisha utarabu wa mtuhumiwa kuachiwa kwa dhamana.
Masharti hayo
yaliyotolewa leo na Jaji Zainabu Mruke muda mfupi baada ya mawakili wa Lulu,
Peter Kibatara, Kennedy Fungamtama na Fulgence Massawe kuiomba mahakama hiyo
impatie dhamana mshtakiwa huyo ambaye anasota rumande tangu April mwaka jana
ambapo walieleza kuwa ombi la dhamana wameliwasilisha chini ya kifungu cha
148(1), (2)
cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002.
Jaji Mruke
alisema ili mahakama impatie dhamana ni lazima asalimishe kwa Msajili wa Mahakama
hiyo hati ya kusafiria, kutotoka nje ya Dar es Salaam bila ruhusa ya Mahakama, kuripoti kwa msajili
kila mwezi, kuwa na wadhamini wawili ambao ni watumishi wa Serikali ambao
watasaini bondi ya Sh. Milioni 20 kila mmoja.
Baada ya
jaji huyo kutangaza masharti hayo Lulu na wakili wake walitoka nje ya ukumbi
uliokuwa ukiendeshwa kwa shauri hilo kwa ajili ya kwenda kwa msajili kutimiza
masharti hayo lakini kwa bahati mbaya Msajili hakuwepo ofisini na hivyo kufanya
Lulu kurudishwa rumande hadi kesho atakapoletwa kwaajili ya kujatimiza masharti
hayo mbele ya Msajili wa mahakama hiyo.
Kufuatia
mahakama hiyo leo kumpatia masharti ya dhamana Lulu kutoka na ombi lake
Na.125/2012 la kuomba mahakama hiyo impatie dhamana, lakini bado kesi ya msingi
inayomkabili Lulu ambayo ni ya kuua bila kukusudia bado haijapangiwa jaji wala
tarehe ya kuanza kusikilizwa.
Desemba 21
mwaka jana , Hakimu Mkazi Christine Mbando wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
aliifunga kesi ya kuua bila kukusudia Lulu na kuiamishia rasmi kesi hiyo katika
Mahakama Kuu, na uamuzi huo wa mahakama ulitokana na upande wa Jamhuri kumsomea
maelezo ya kesi yake kwa kina mshtakiwa huyo na kuieleza mahakama kuwa
wanakusudia kuleta jumla ya mashahidi tisa.