MZUNGUKO wa
pili wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ambayo itatoa timu tatu zitakazocheza Ligi
Kuu ya Vodacom (VPL) msimu ujao (2013/2014) unaanza Jumamosi (Februari 2 mwaka
huu) katika viwanja tisa tofauti.
Kundi A
litakuwa na mechi kati ya Mbeya City na Burkina Faso itakayochezwa Uwanja wa
Sokoine jijini Mbeya, Majimaji na Kurugenzi katika Uwanja wa Majimaji mjini
Songea, na Polisi Iringa dhidi ya Mkamba Rangers kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya
Samora mjini Iringa.
Mechi za
Kundi B, Jumamosi (Februari 2 mwaka huu) itakuwa Transit Camp na Ndanda
itakayochezwa Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani, Moro United dhidi ya Villa Squad
(Uwanja wa Karume, Dar es Salaam). Jumapili (Februari 3 mwaka huu) ni Tessema
na Green Warriors (Mabatini, Pwani), Ashanti United na Polisi Dar (Uwanja wa
Karume, Dar es Salaam).
Kundi C
Jumamosi (Februari 2 mwaka huu) ni Polisi Dodoma na Kanembwa JKT (Uwanja wa
Jamhuri, Dodoma), Morani dhidi ya Mwadui (Uwanja wa Kiteto, Manyara), Polisi
Mara na Pamba (Uwanja wa Karume, Musoma), Polisi Tabora na Rhino Rangers
(Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora).
Ligi hiyo
inatarajiwa kumalizika mwishoni mwa Machi mwaka huu ambapo mshindi wa kila
kundi atapanda daraja kucheza Ligi Kuu msimu ujao. (Ratiba imeambatanishwa)