Dina Ismail, mmoja wa Wajumbe kamati ya Tuzo |
Na Princess Asia
CHAMA Cha
Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), kimeanza mchakato wa Tuzo kwa
Wanamichezo Bora wa Tanzania mwaka 2012.
Katibu Mkuu
wa TASWA, Amir Mhando amesema kama ilivyokuwa mwaka uliopita Kamati ya Utendaji
ya TASWA imeamua suala la mchakato wa kuwapata wanamichezo hao lifanywe na
kamati maalum nje ya Kamati ya Utendaji ya TASWA lengo ikiwa ni kupanua wigo na
kuwashirikisha wadau wengi zaidi katika jambo hili nyeti.
Amesema jukumu
la Kamati ya Utendaji ya TASWA itakuwa ni kuhangaika na mambo ya wadhamini na
masuala mengine yahusuyo sherehe hizo ambazo tunataka ziwe za aina yake.
Kutokana na
hali hiyo Kamati ya Utendaji ya TASWA iliyokutana wiki iliyopita iliteua kamati
maalum ya watu 11 kusimamia mchakato wa kuwapata wanamichezo hao, ambapo kamati
hiyo inayotarajia kuanza vikao vyake Jumatano Januari 30, 2013 itakuwa chini ya
uenyekiti wa mwanachama wa TASWA, Haji Manara.
Kamati ya
Utendaji imemkabidhi jukumu Manara baada ya kujiridhisha pasi na shaka uzoefu
wake katika masuala ya michezo na pia uzoefu wake katika mambo mbalimbali ya
kiutawala, hivyo kuwa na imani kwamba ataendesha vizuri mchakato kama
walivyofanya watangulizi wake.
Wajumbe saba
wa kamati hiyo wanatoka nje ya Kamati ya Utendaji ya TASWA ambao ni Jane John,
Dina Ismail, Jabir Idrissa, Tulo Chambo,
Abdallah Mweri na ofisa mmoja ambaye ataombwa kutoka Baraza la Michezo la Taifa
(BMT), wakati wajumbe wanne wanatoka Kamati ya Utendaji ya TASWA ambao ni Grace
Hoka, Zena Chande, Alfred Lucas na Amir Mhando