Kiiza |
Na Mahmoud Zubeiry
KIPA wa tatu
wa Yanga SC, Yussuf Abdul na mshambuliaji Mganda, Hamisi Kiiza ‘Diego’
waliokuwa wanasumbuliwa na Malaria, wamepona na leo wamefanya mazoezi na wenzao
kwenye Uwanja wa Mabatini, Kijitonyama, Dar es Salaam.
Wawili hao
walikosa mchezo wa kujipima nguvu dhidi ya Black Leopard ya Afrika Kusini juzi
kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, ambao timu yao ilishinda mabao 3-2.
Ofisa Habari
wa Yanga, Baraka Kizguto ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, timu
imeendelea na mazoezi leo na wachezaji wote wameshiriki wakiwemo Abdul na
Kiiza.
Alisema kwa
sasa Yanga haina majeruhi hata mmoja na inaendelea vema na mazoezi yake
kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu hya Vodacom Tanzania Bara unaoanza
mwishoni mwa wiki.
Mabingwa hao
wa Afrika Mashariki na Kati, katika kujiandaa na mzunguko huo wa pili wa Ligi
Kuu, waliweka kambi ya wiki mbili Jijini Antalya, Uturuki kuanzia Desemba 30
mwaka jana hadi Januari 12 mwaka huu.
Katika kambi
hiyo, pamoja na kufanya mazoezi ya nguvu ya ufukweni, uwanjani na gym, Yanga
ilipata mechi tatu za kujipima nguvu dhidi ya Ariminia Bielefed ya Daraja
la Nne Ujerumani waliyotoka nayo sare ya 1-1, kabla ya kufungwa 2-1 na Denizlispor FC ya
Daraja la Kwanza Uturuki na 2-0 na Emmen FC ya Daraja la Kwanza Uholanzi.
Yanga ilimaliza
mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu, ikiwa inaongoza ligi hiyo kwa pointi zake 29,
baada ya kucheza mechi 13, ikifuatiwa na Azam iliyomaliza na pointi zake 24 na
mabingwa watetezi, Simba SC waliomaliza na pointi 23.
MSIMAMO WA LIGI KUU YA VODACOM
2012/2103:
1 Yanga 13 9 2 2 25 10 15 29
2 Azam 13 7 3 3 17 11 6 24
3 Simba SC 13 6 5 2 20 11 9 23
4 Mtibwa Sugar 13 6 4 3 18 12 6 22
5 Coastal Union 13 6 4 3 16 14 2 22
6 Kagera Sugar 13 5 6 2 15 10 5 21
7 Ruvu Shooting 13 6 2 5 19 17 2 20
8 Mgambo JKT 13 5 2 6 10 13 -3 17
9 JKT Ruvu 13 4 3 6 13 20 -7 15
10 JKT Oljoro 13 3 5 5 13 16 -3 14
11 TZ Prisons 13 3 5 5 8 12 -4 14
12 Toto African 13 2 6 5 10 15 -5 12
13 African Lyon 13 2 3 8 9 20 -11 9
14 Polisi Moro 13 0 4 9 4 16 -12 4