Kado |
Na Boniface Wambura
KAMATI ya
Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ilikutana Januari 19 mwaka huu kupitia
maombi ya usajili wa dirisha dogo kwa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na
Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ambapo kipa Shabani Kado ameidhinishwa kuidakia
timu ya Coastal Union ya Tanga.
Wachezaji
wengine waliodhinishwa kwenye dirisha dogo na klabu zao kwenye mabano ni
Humphrey Mieno, Brian Umony, Jockins Atudo, David Mwantika, Abdallah Seif,
Malika Ndeule na Uhuru Selemani- kwa mkopo (Azam), Juma Mdindi, Njaidi Mohamed
na Mahmoud Mbulu (Ruvu Shooting), Mohamed Kayi na Emmanuel Gabriel (Tanzania
Prisons).
Nurdin
Selemani, Shaibu Nayopa, Hamidu Hassan, Paul Malipesa, Josephat Moses, Muharami
Mnyangamala, Majaliwa Mbaga na Alphonce Peter (Oljoro JKT), Shukuru Kassim,
Chacha Marwa, Salum Machaku, Mzamiru Said, Victor Bundala, Delta Thomas, Edward
Mzeru na Tizzo Chomba (Polisi Morogoro), Edmund Kashamila na Julius Mrope
(Kagera Sugar).
Rajab
Mohamed, Zakayo Joseph, Baraka Anthony na Mussa Chambo (Mtibwa Sugar), Zahoro
Pazi- kwa mkopo, Emmanuel Linjechele, Kisimba Luambano na Nashon Naftali (JKT
Ruvu), Moaka Shabani, Ismail Mkaima na Damas Milanzi (Mgambo Shooting), Donald
Obimma, Exavery Muhollery, Mohamed Hussein na Ulugbe Odia (Toto Africans).
Obadi
Mungusa, Juma Seif, Yusuf Mgwao, Ibrahim Job- kwa mkopo, Shamte Ally- kwa
mkopo, Buya Jamwaka, Takang Valentine, Nurdin Mussa, Salvatory Jackson, Mohamed
Athuman, Athuman Kajembe na Jarufu Kizombi (African Lyon), Mussa Mudde na Abel
Dhaila (Simba).
Rashid
Simba, Zuberi Hamisi, Shaongwe Ramadhan, Castory Mumbara, Tinashe Machemedze na
Shabani Kado (Coastal Union).
Mchezaji
Martin Mlolere aliyeombewa usajili Mgambo Shooting kutoka Majimaji amekataliwa
kwa vile taratibu za uhamisho hazijakamilika, hivyo anabaki kwenye timu yake ya
Majimaji.