Kocha Mkuu wa Simba SC, Patrick Liewig akiwa na
Msaidizi wake Jamhuri Kihwelo. Wawili hawa wamezoana kwa haraka na kuwa
marafiki wakubwa, jambo ambalo linaashiria watafanya kazi kwa ushirikiano na
ufanisi mkubwa. Raha jinsi wanavyotaniana hapa katika hoteli ya Zanzibar Ocean
View walipofikia, kushirikiana na walivyo bega kwa bega. Liewig anaanza kazi
rasmi leo jioni visiwani hapa, baada ya jana kuishuhudia timu ikimenyana na
Jamhuri ya Pemba katika mechi ya ufunguzi ya Kombe la Mapinduzi na kushinda
mabao 4-2. Kuhusu usafiri, ‘Samjo’ Julio
tayari amekwishaingia kwenye kona zake na kaibuka na mkoko mmoja wa hatari,
full time wanakula kiyoyozi na bosi wake wakikatiza mitaa ya Zanzibar kwenda
mazoezini na kwenye mechi. Baab kubwa. |