Na Prince Akbar
KAMATI ya
maandalizi ya Fainali ya tuzo za Mwanasoka Bora wa mwaka (Wazalendo Footballer
of the Year), imekamilisha mchakato wa kupitisha majina ya wanasoka walioingia
katika fainali ya tuzo hizo mwaka 2012.
Taarifa ya
Mratibu, Ahadi Kakore imesema katika mchakato huo kamati iliweza kuangalia vigezo vikuu vinne ambavyo ndivyo vitaendelea
kuwa dira na mwongozo hadi siku ya fainali Januari 31 mwaka 2013.
“Awe ni
mchezaji wa timu ya taifa, mchango wake
katika klabu yake na timu ya taifa, nidhamu kwa ujumla ndani na nje ya uwanja
na asiwe na kashfa ya utumiaji wa dawa zilizopigwa marufuku michezoni ikiwemo
dawa za kulevya,”imesema taarifa hiyo.
Taarifa ya
Kakore imesema wapo wachezaji ambao hawajaweza kuwa na vigezo vyote lakini
akawa navyo viwili kati ya hivyo aliweza kupita. Kwa mfano wapo wachezaji ambao
uwezo wao ni wa hali ya juu ambapo wanastahili kucheza timu ya taifa lakini
wameshindwa kupata nafasi kutokana na sababu mbalimbali lakini uwezo wake hauna
shaka hivyo ni ngumu kumtoa kwenye kinyang’anyiro hiki.
Tuzo hizo
zimegawanyika katika makundi tofauti tofauti ambapo jumla ya tuzo zote ni 12
kutokana na ukweli kwamba katika tuzo za maendeleo ya soka la wanawake zipo
tuzo mbili ya wanaume na wanawake.
Mgawanyo wa
tuzo hizo ni kama ifuatavyo; Kipa Bora, Beki Bora, Kiungo Bora, Mshambuliaji
Bora, Mchezaji anayechipukia, Mchezaji Bora wa Kike, Mchezaji Bora Kigeni,
Mchezaji bora wa zamani, Maendeleo soka la Wanawake, Mwanasiasa wa Afrika
aliyesadia maendeleo ya michezo pamoja na tuzo kubwa ya Mwanasoka Bora wa mwaka
2012. Fainali ya hizo zitafanyika Januari 31 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
WALIOPITISHWA
KUWANIA TUZO:
Kundi A:
Kipa Bora
Mwandini
Ally- Azam FC, Juma Kaseja- Simba, Shaaban Kado- Mtibwa Sugar, Ally
Mustapha-Yanga, Jackson Chove-Coastal Union, Deogratius Munishi- Azam FC
Kundi B:
Beki Bora
Nassor Said
– Simba, Nadir Haroub – Yanga, Agrey Morris- Azam FC, Amir Maftah- Simba,
Kelvin Yondan-Yanga na Shomari
Kapombe-Simba.
Kundi C:
Kiungo Bora
Shaban Nditi
–Mtibwa, Frank Domayo- Yanga, Mwinyi Kazimoto-Simba, Amri Kiemba-Simba, Chande
Mgoja- Mgambo JKT na Abubakar Salum-Azam FC.
Kundi D:
Mshambuliaji Bora
John Bocco -
Azam FC, Mrisho Ngassa – Simba, Hussein Javu -Mtibwa FC, Amiry Omary-JKT
Oljoro, Simon Msuva-Yanga, Nsa Job-Coastal Union.
Kundi E:
Mchezaji anayechipukia
Mudasir
Yahya-Azam FC, Ramadhan Singano-Simba, Edward Christopher-Simba, Manyika Peter
Manyika- Mgambo JKT, Miraji Adam-Simba na Chande Mgoja- Mgambo JKT
Kundi F:
Mchezaji Bora wa Kike
Ester
Chabruma-Sayari Queens, Mwanahamisi Omar-Mburahati Queens, Mwapewa Mtumwa-Ever
Green, Fatuma Mustafa-Sayari Queens, Asha Rashid-Mburahati Queens na Sophia
Mwasikili-Luleburgaz Spor Kulubu- Uturuki.
Kundi H:
Mchezaji Bora wa mwaka 2012
Mchezaji
atakayetwaa tuzo hii atatoka katika makundi yaliyotajwa hapo juu hii ikiwa na
maana kwamba kuanzia kundi A-E. hii ni kumaanisha kuwa wanawake hawataingia
kwenye kundi hili wala kwa sababu tayari wanayio tuzo yao tayari kama
inavyoonekana katika kipengele F.
Kundi I:
Mchezaji Bora Kigeni
Haruna
Niyonzima-Yanga, Kipre Tchetche-Azam FC, Emmanuel Okwi-Simba, Felix Sunzu-Simba, Hamis Kiiza-Yanga na Jerry
Santo-Coastal Union.
TUZO ZA
HESHIMA
Kundi H:
Mchezaji bora wa zamani
Madaraka
Suleiman – Simba, Edibily Lunyamila-Yanga/Simba/Twiga FC,
Mohamed
Mwameja-Simba, Yusuf Macho-Simba/Kagera Sugar, Zamoyoni Mogela-Simba/Yanga na
Kenny Mkapa-Yanga.
Kundi I:
Maendeleo soka la Wanawake (tuzo mbili Mwanamke na Mwanaume)
Stephania
Kubumba-Sayari, Arafa Tamba-Mburahati Queens, Fatma Makambara-Sayari, Pili
Kambangwa- Mchangani, Joha Halfan-Vijana Queens, Amin Bakhresa, Frenk Mchaki
na Idd Azan.
Kundi
J:Mwanasiasa wa Afrika aliyesadia maendeleo ya michezo
Benjamin
Mkapa-Tanzania, Daniel Arap Moi-Kenya na Joachim Chisano-Msumbiji
Katika
kipengere hiki ni kwamba kilichoangaliwa ni namna gani mwanasiasa mstaafu
alivyweza kusaidia michezo kwa ujumla ikiwemo soka. Hapa inaangaliwa ujewekaji
wa miundo mbinu, kama ujezi wa viwanja vya michezo, mafanikio katika klabu
na timu za taifa katika nchi ambayo
amekuwa akiiongoza.
Pia
kipengere hiki pia kinaangalia katika kipindi kisichozidi miaka 10 ya utawala
akiwa kama mkuu wa nchi husika.
Baada ya
kufuatilia kwa takriban mwaka mmoja katika nchi zilizopo jirani na Tanzania,
imeonekana wazi kuwa viongozi hao wastaafu ndiyo wenye waliofikia viwango
ambavyo kamati ilivihitaji.