Ally Mohamed
‘Gaucho’ akipambana na wachezaji wa Coastal Union, Othman Tamim na Suleiman
Kassim ‘Selembe’ katika mchezo wa leo wa Kundi B, Kombe la Mapinduzi kwenye
Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
|
Na Mahmoud Zubeiry, Zanzibar
COASTAL
Union ya Tanga imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Mtibwa Sugar ya
Morogoro, katika mchezo wa Kundi B Kombe la Mapinduzi, jioni hii kwenye Uwanja
wa Amaan visiwani hapa.
Hadi
mapumziko, hakuna timu iliyofanikiwa kuona lango la mwenzake na Coastal Union
ndio walitakiwa kujilaumu kwa kushindwa kutumia mwanya wa Mtibwa Sugar kucheza
pungufu kutokana na beki wake, Salum Swedi kutolewa nje kwa kadi nyekundu
dakika ya 43.
Timu
zilishambuliana kwa zamu katika kipindi hicho, upande wa Coastal ukiongozwa na
Danny Lyanga na Mtibwa Hussein Javu.
Baada ya
Swedi kutolewa nje kwa kadi nyekundu, kocha Mecky Mexime alimuinua beki Rajab
Mohamed kwenda kuchukua nafasi ya mshambuliaji, Hassan Seif.
Kipindi cha
pili, Mtibwa walirudi kwa kasi na kufanikiwa kupata bao la kuongoza dakika ya
58, mfungaji Ally Mohamed ‘Gaucho’ aliyepiga shuti la umbali wa mita 19 na
kumtungua Juma Mpongo.
Coastal Union
ilisawazisha bao hilo dakika ya 81, mfungaji Jerry Santo aliyefumua shuti la
chini la umbali wa mita 24 na kumtungua kipa Hussein Sharrif.
Katika mchezo
huo, kikosi cha Mtibwa Sugar kilikuwa; Hussein Sharrif, Hamisi Issa, Yussuf Nguya,
Salvatory Ntebe, Salum Swedi, Babu Ally Seif, Ally Mohamed ‘Gaucho’, Rashid
Gumbo, Hussein Javu, Hassan Seif/Rajab Mohamed dk43 na Vincent Barnabas.
Coastal
Union; Juma Mpongo, Ismail Khamis, Othman Tamim, Philip Metusela, Mbwana Khamis
‘Kibacha’, Hamisi Shengo, Suleiman Kassim ‘Selembe’, Jerry Santo, Mohamed
Miraj, Mohamed Soud Othman na Danny Lyanga.
MSIMAMO WA KUNDI B:
P W D L GF
GA GDPts
Miembeni 1 1 0 0 4 1 3 3
Coastal
Union 2 0 2 0 1 1 0 2
Mtibwa Sugar 2 0 1 1 2 5 -3 1
Azam FC 1 0 1 0 0 0 0 1