Azam FC
jioni hii imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Toto Africans ya Mwanza
katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodadom Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa
Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Mabao ya
Azam katika mchezo huo yametiwa kimiani na Kipre Michael Balou wa Ivory Coast, dakika
ya tisa, Mganda, Brian Umony dakika ya 20 na Mkenya Humphrey Mieno dakika ya
46, wakati bao l kufutia machozi la Toto lilifungwa na Selemani Kibuta dakika ya
77.
Ushindi huo,
unaifanya Azam ifikishe pointi 30, baada ya kucheza mechi 15, ikizidiwa mbili
na Yanga inayoongoza kwa pointi zake 32, ingawa imecheza mechi 14.
|