Mwenyekiti wa ZFA, Aman Ibrahim Makungu, waandaaji wa Kombe la Mapinduzi |
Na Mahmoud Zubeiry, Zanzibar
MICHUANO ya
Kombe la Mapinduzi inatarajiwa kuendelea leo kwenye Uwanja wa Amaan mjini hapa,
kwa michezo miwili ya Kundi B, baada ya mechi mbili za jana za Kundi A
kushuhudia mvua ya mabao.
Mapema saa
10:30, mabingwa wa zamani wa Kombe hilo watakutana, Mtibwa Sugar ya Morogoro waliotwaa
taji hilo mwaka 2003 na 2010 dhidi ya Miembeni ya hapa waliotwaa taji hilo mwaka 2009,
kabla ya mabingwa watetezi, Azam FC ya Dar es Salaam kushuka dimbani saa 2:00
usiku kumenyana na Coastal Union ya Tanga inayoshiriki mashindano haya kwa mara
ya kwanza.
Juma Jabu wa Coastal akikimbizwa na Kipre Tchetche wa Azam timu hizo zilipokutana katika Ligi Kuu mwaka jana mzungukowa kwanza. Coastal ilipigwa 4-1. Leo itakuwaje Amaan? |
Katika mechi
za ufunguzi jana, mabingwa wa Tanzania Bara, Simba SC walianza vyema michuano hiyo
baada ya kuwachapa mabingwa wa Zanzibar, Jamhuri ya Pemba mabao 4-2 usiku,
wakati mabingwa wa Kenya, Tusker waliitandika Bandari ya hapa mabao 5-1.
Katika mechi
ya Simba na Jamhuri, hadi mapumziko, timu hizo zilikuwa zimekwishafungana mabao
2-2, zikicheza huku zikinyeshewa na mvua iliyoanza kabla hazijaingia uwanjani.
Jamhuri ndio
waliokuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 17, mfungaji Mfanyeje Mussa Yussuf kwa
shuti la umbali wa mita 17.
Simba
ilisawazisha bao hilo dakika ya 27, mfungaji Haruna Athumani Chanongo
aliyeunganisha kwa kichwa kona maridadi iliyochongwa na kiungo Kiggi Makassy
kutoka wingi ya kulia.
Baada ya bao
hilo, Simba walizidisha mashambulizi langoni mwa Jamhuri na iliwachukua dakika
mbili zaidi kupata bao la kuongoza, baada ya Chanongo kufumua shuti kali akiwa
umbali wa mita 20 upande wa kushoto mwa Uwanja, ambalo lilimshinda mlinda
mlango Jaffar Said.
Huku
ikielekea kama Simba itatoka uwanjani baada ya ngwe ya kwanza ikiwa inaongoza
2-1, Mfanyeje tena aliwainua vitini wapenzi wa timu hiyo ya Chasasa, Pemba kwa
bao tamu la kusawazisha akimalizia mpira wa adhabu uliopigwa na Abdallah
Athumani, akamtungua kiulaini kipa wa Simba, William Mweta.
Kipindi cha
pili, Simba walirudi kwa kasi ya kusaka bao la ushindi iliwachukua dakika 12 tu
kufanikisha malengo yao, baada ya Nahodha wa timu hiyo leo, Shomary Kapombe
aliyecheza kama kiungo mkabaji badala ya beki wa kati, kufunga kwa shuti la
chini la mpira wa adhabu.
Adhabu hiyo
ilifuatia mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia, Felix Mumba Sunzu Jr. kufanyiwa madhambi nje kidogo ya eneo la
hatari na beki mmoja wa Jamhuri.
Sunzu
aliwainua vitini wapenzi wa Simba dakika ya 66, baada ya kuuwahi mpira uliokuwa
unaelekea kutoka nje na kugeuka nao kuutumbukiza nyavuni kiufundi.
Kabla ya
mchezo huo, Makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar, Seif Sharrif Hamad alizindua
mashindano hayo kwa kupiga penalti na kumfunga kipa wa Jamhuri, Jaffar.
Akiongozwa na raisi wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), Aman Ibrahim Makungu, Mh
Seif ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CUF, alizikagua timu zote mbili kabla ya
kuanza kucheza.
Kocha mpya
wa Simba, Mfaransa Patrick Liewig alikuwa jukwaani akiishuhudia timu,
ikiongozwa na watakaokuwa wasaidizi wake, Mganda Moses Basena na mzalendo,
Jamhuri Kihwelo.
Katika
mchezo wa leo, kikosi cha Simba SC kilikuwa; William Mweta, Miraj Adam, Paul
Ngalema, Mussa Mudde/Abdallah Seseme dk81, Komabil Keita, Shomary Kapombe,
Haroun Chanongo, Mwinyi Kazimoto/Jonas Mkude 67, Felix Sunzu/Ramadhan Singano
dk81, Haruna Moshi na Kiggi
Makassy/Christopher Edward dk27.
Jamhuri FC;
Jaffar Said/Suleiman Maabad dk 75, Msafiri Leonard, Hamad Omar, Hussein Omar,
Mfaume Shaaban, Soud Amoud, Bakari Hamisi, Ally Bilal/Mbara Ali dk82, Ally
Ahmed ‘Shiboli’, Mfanyeje Mussa na Abdallah Athumani.
Katika
mchezo uliotangulia, Tusker ya Kenya iliichapa Bandari ya hapa mabao 5-1, mabao
ya Jesse Were 29 na 43, Ismail Dunga 35 Michael Olunga dakika ya 89 na Andrew
Tolowa dakika ya 90, wakati la Bandari lilifungwa na Amour Janja dakika ya 83.
MSIMAMO WA
KUNDI A:
P W D L GF GA GDPts
Tusker FC 1 1 0 0 5 1 4 3
Simba SC 1 1 0 0 4 2 2 3
Jamhuri FC 1 0 0 1 2 4 -2 0
Bandari FC 1 0 0 1 1 5 -4 0
MSIMAMO WA
KUNDI A:
P W D L GA
GF GDPts
Azam FC 0 0 0 0 0 0 0 0
Mtibwa Sugar 0 0 0 0 0 0 0 0
Coastal
Union 0 0 0 0 0 0 0 0
Miembeni 0 0 0 0 0 0 0 0
RATIBA KOMBE
LA MAPINDUZI:
Janauri 2, 2013
Tusker 5-1
Bandari
Simba SC 4-2
Jamhuri
Januari 3, 2013
Mtibwa Sugar
Vs Miembeni
Azam FC Vs
Coastal Union
Januari 4, 2013
Jamhuri Vs
Bandari
Simba SC Vs
Tusker FC
Januari 5, 2013
Mtibwa Sugar
Vs Coastal Union
Miembeni Vs
Azam
Januari 6, 2013
Tusker vs
Jamhuri
Simba SC Vs
Bandari
Januari 7, 2013
Miembeni Vs
Coastal Union
Azam FC Vs
Mtibwa Sugar
Januari 9, 2013
Nusu Fainali
ya kwanza
Januari 10, 2013
Nusu Fainali
ya pili
Januari 12,
2013
FAINALI
ORODHA YA MABINGWA KOMBE LA MAPINDUZI
2003 Mtibwa Sugar
2004 Yanga SC
2005 Yanga SC
2006 Simba SC
2007 Yanga SC
2008 Simba SC
2009 Miembeni FC
2010 Mtibwa Sugar
2011 Simba SC
2012 Azam FC
2012 Azam FC