Na Mahmoud Zubeiry,
Zanzibar
AZAM FC na
Coastal Union ya Tanga zimetoshana nguvu baada ya kutoka sare ya bila kufungana
katika mchezo wa Kundi B, Kombe la Mapinduzi usiku huu kwenye Uwanja wa Amaan,
visiwani hapa.
Coastal leo
ndio waliotawala mchezo na kupoteza nafasi kama tatu za wazi za kufunga mabao,
kutokana na umakini mdogo kila walipopata nafasi hizo.
Azam walipata
nafasi moja nzuri kipindi cha pili, lakini walinzi wa Coastal walisimama imara
na kuondosha kwenye hatari jaribio hilo.
Katika mchezo
huo, kikosi cha Azam FC kilikuwa; Mwadini Ally, Himid Mao, Samir Hajji Nuhu,
David Mwantika, Joackins Atudo, Kipre Balou, Salum Abubakar, Humphrey Mieno,
Gaudence Mwaikimba, Kipre Tchetche/Brian Umony dk 24 na Hamisi Mcha ‘Vialli’/Seif
Abdallah dk 66.
Coastal
Union; Juma Mpongo, Ismail Khamis, Othman Tamim, Philip Metusela, Mbwana Khamis
‘Kibacha’, Hamisi Shengo, Suleiman Kassim ‘Selembe’/Hussein Twaha dk 50, Jerry
Santo, Mohamed Mtindi, Soud Othman/Razack Khalfan dk90 na Danny Lyanga/Joseph
Mahundi dk 90.
Katika
mchezo wa kwanza wa kundi hilo, Miembeni iliitandika mabao 4-1 Mtibwa Sugar
kwenye Uwanja wa mao Dze Tung.
Mabao ya
Miembeni yalitiwa kimiani Adeyum Saleh Ahmed dakika ya 41 na 72, Mohamed
Hamdani na Rashid Roshwa dakiaka ya 74, wakati la Mtibwa la kufutia machozi
lilifungwa na Juma Mpakala dakika ya 10.