Klabu ya Young Africans leo imeingia mkataba na kampuni ya Prime Time Promotions ya jijini Dar es saaalm kwa ajili ya kuandaa shuguli za mkutano mkuu wa wanachama utakaofanyika Januari 19, 2013 ambapo kampuni ya Prime Time imetoa mil 105,000,000 kwa ajili ya kuratibu shughuli hiyo.
Akiongea na waandishi wa habari, makamu mwenyekiti wa klabu ya Yanga Clement Sanga amesema wamefikia hatua hiyo kuipa nafasi kampuni ya Prime Time kuweza kuuendesha mkutano huo kisasa zaidi, ambapo unategemewa kufanyika na kuonyesha moja kw amoja (live) kupitia kituo cha Luninga ya Clouds.
Prime Time pia imepewa fursa ya kusaka masoko na wadhamini wa klabu ya Yanga ili kuhakikisha klabu inajijenga vizuri kiuchumi kwa kubuni miradi mbali mbali, ambapo kwa kuanzia itaanda mchezo mmoja wa kirafiki na timu kubwa barani Afrika mwanzoni mwa mwezi Januari 2013.
Naye Mkurugenzi wa Prime Time Promotions Joseph Kusaga amesema amefurahishwa kwa kampun yake kupewa nafasi hiyo na kusema wanaahidi watafanya kazi nzuri kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Aidha Kusaga alisema milango iko wazi kwa timu yoyote kuomba kushirikiana nao, kwani hawana itikadi ya timu yoyote bali lengo lao ni kufanya timu zote ziwe katika nafasi nzuri kiuchumi na kujitangaza kimichezo na kimasoko.