Na Prince Akbar
MICHUANO ya
kuwania Kombe la Uhai inayoshirikisha wachezaji wenye umri chini ya miaka 20 wa
klabu za Ligi Kuu ya Vodacom, inatarajiwa kuendelea leo kwa mechi Kundi C
kupigwa.
Kagera Sugar
itacheza na Oljoro JKT saa 8 mchana- Karume wakati Yanga na Ruvu Shooting
zitakuwa kwenye Uwanja wa Chamazi kuanzia saa 10 kamili jioni. (Ratiba nzima
imeambatanishwa)
Timu zinazoshiriki
michuano hiyo iliyoanza jana na itamalizika Desemba 23, mwaka huu., zimegawanywa
katika makundi matatu, Kundi A likiwa na timu za Coastal Union, JKT Ruvu,
Mtibwa Sugar, Tanzania Prisons na Toto Africans, Kundi B ni African Lyon, Azam,
Mgambo Shooting, Polisi Morogoro na Simba, wakati timu za Kagera Sugar, Oljoro
JKT, Ruvu Shooting na Yanga zinaunda kundi C.
Katika mechi
za jana, Azam FC ilianza vema baada ya kuilaza Mgambo Shooting mabao 2-0 jioni
ya leo kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam, shukrani kwao,
Jamil Mchaulu ‘Balotelli’ na Reyna Mgugingila, wafungaji wa mabao hayo leo
katika mchezo huo wa Kundi B.
Katika mechi
za asubuhi jana, Coastal Union ya Tanga nayo ilianza vizuri baada ya kuifunga
Tanzania Prisons mabao 2-1, mchezo wa Kundi A uliopigwa Uwanja wa Karume, Dar
es Salaam.
Coastal
Union ilimaliza kipindi cha kwanza ikiwa tayari imepachika mabao hayo
yaliyofungwa dakika ya 24 na 33 kupitia kwa Ramadhan Same na Yusuf Chuma na
African Lyon iliichapa mabao 4-0 Polisi Moro.