![]() |
Uwanja wa Ndege wa Istanbul ambako Yanga wapo kwa sasa |
Na Mahmoud Zubeiry
YANGA SC, mabingwa
mara tano wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame wamefika
salama Istanbul, Uturuki kiasi cha saa moja iliyopita na sasa wanasubiri ndege
ya kuunganisha kwenda Antalya, ambako wataweka kambi.
Mwenyekiti wa
Kamati ya Mashindano ya Yanga, Abdallah Ahmad Bin Kleb ameiambia BIN
ZUBEIRY mida hii kwamba, amewasiliana na Mkuu wa Msafara, Mohamed
Nyenge kampa taarifa hizo.
Yanga
itaweka kambi katika mji wa Antalya uliopo kusini mwa Uturuki na itafikia
katika hoteli ya Sueno Beach iliyopo pembezoni mwa bahari ya Meditreanian, na
itakua ikifanya mazoezi katika viwanja vikubwa viwili vilivyopo katika hotel
hiyo na kiwanja kidogo cha nyasi bandia.
Yanga iliondoka
Dar es Salaam Alfajiri ya leo, saa 10:30 ikiwa na kikosi kamili; makipa; Ally
Mustafa 'Barthez', Said Mohamed na Yussuf Abdul, mabeki Juma Abdul, Shadrack
Nsajigwa, Godfrey Taita, Stefano Mwasyika, Oscar Joshua, Mbuyu Twite, Nadir
Haroub ‘Cannavaro’, Ladisalus Mbogo na Kelvin Yondani.
Viungo ni Athumani
Iddi ‘Chuji’, Frank Domayo, Haruna Niyonzima, Kabange Twite, Nurdin Bakari, Omega
Seme, Simon Msuva, Rehani Kibingu, Nizar Khalfani na David Luhende wakati washambuliaji
ni Didier Kavumbagu, Said Bahanunzi, Jerry Tegete, George Banda na Hamisi Kiiza.
Upande wa
benchi la ufundi ni Kocha Mkuu Mholanzi, Ernie Brandts, Kocha Msaidizi Freddy
Felix Minziro na Kocha wa makipa, Razak Ssiwa, na Maofisa wengine ni Daktari wa
timu, Sufiani Juma, Meneja Hafidh Saleh, Ofisa Habari, Baraka Kizuguto Mjumbe
wa Kamati ya Utendaji, Mohammed Nyenge.