// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); YANGA KUPAA DESEMBA 28, KULA MWAKA MPYA ULAYA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE YANGA KUPAA DESEMBA 28, KULA MWAKA MPYA ULAYA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, December 16, 2012

    YANGA KUPAA DESEMBA 28, KULA MWAKA MPYA ULAYA


    Kocha Brandts na wachezaji wake
    Na Prince Akbar
    MABINGWA wa soka Afrika Mashariki na Kati, Yanga SC wanatarajiwa kuondoka Desemba 28, mwaka huu mjini Dar es Salaam, kwenda Uturuki kuweka kambi ya wiki mbili kujiandaa kwenda kutetea taji lao hilo mjini Kigali, Rwanda.
    Habari kutoka ndani ya Yanga, zimesema kwamba wiki hii mwalimu, Ernie Brandts ataamua idadi na wachezaji wa kwenda ziara hiyo, ambayo ni maalum pia kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu.
    Kocha huyo Mholanzi, kwa wiki zaidi ya mbili amekuwa akikinoa kikosi chake kwenye Uwanja wa sekondari ya Loyola, Dar es Salaam baada ya kumaliza likizo fupi ya baada ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu.
    Yanga, chini ya Mwenyekiti wake, Alhaj Yussuf Manji imepania kurejesha utawala wake katika soka ya Tanzania na kwa kuanzia inataka kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu kwa kishindo mwishoni mwa msimu.
    Yanga inataka pia kutetea Kombe la Kagame Januari mwakani mjini Kigali, katika michuano ambayo watakwenda na wapinzani wao wa jadi, Simba SC.
    Yanga ilimaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ikiwa inaongoza kwa pointi zake 29, ikifuatiwa na Azam yenye pointi 24, wakati Simba ni ya tatu kwa pointi zake 23.     

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: YANGA KUPAA DESEMBA 28, KULA MWAKA MPYA ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top