Stars |
Na Prince Akbar
REFA
Sylvester Kirwa kutoka Kenya ndiye atakayechezesha mechi ya kirafiki ya
kimataifa kati ya Taifa Stars na mabingwa wa Afrika, Zambia (Chipolopolo)
itakayofanyika Desemba 22 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kirwa
anayetambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) atasaidiwa
na Elias Wamalwa na Marwa Range. Waamuzi hao wasaidizi ambao vilevile watatoka
Kenya pia wanatambuliwa na FIFA.
Taifa Stars
inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager tayari iko kambini hoteli ya Tansoma,
na inafanya mazoezi katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume na ule wa Uwanja wa
Taifa kwa ajili ya mechi hiyo inayotarajiwa kuwa na msisimko wa aina yake.