Umony |
Na Mahmoud Zubeiry,
Kinshasa
MSHAMBULIAJI
wa kimataifa wa Uganda, Brian Umony atajiunga na klabu yake mpya, Azam FC baada
ya sikukuu za Krisimasi na mwaka mpya, imeelezwa.
Katibu wa
Azam FC, Nassor Idrisa ameiambia BIN ZUBEIRY mjini hapa kwamba, Umony
ameomba aje kuanza kazi baada ya sikukuu na uongozi umemkubalia.
Azam
inatarajiwa kuondoka hapa mapema Jumatatu kurejea Dar es Salaam baada ya
kumalizika kwa mashindano ya Kombe la Hisani mjini hapa Jumapili.
Nassor
amesema timu ikirejea Dar es Salaam wachezaji watapewa mapumziko ya siku mbili
kwa ajili ya sikukuu na baada ya hapo, watarudi kambini tayari kwa safari ya
Zanzibar kwenye Kombe la Mapinduzi.
Azam ambao
ndio mabingwa watetezi wa Kombe la Mapinduzi, leo watacheza mechi ya Nusu
Fainali na Shark FC Uwanja wa Martyrs na Jumapili watacheza mechi ya mwisho,
iwe ya kusaka mshindi wa tatu au ubingwa, itategemea na matokeo ya leo.