Brian Umony, kifaa kipya Azam |
Na Mahmoud Zubeiry
MSHAMBULIAJI
wa Uganda, Brian Umony ametua Azam FC ya Dar es Salaam kwa mkataba wa miaka
miwili, akitokea KCC ya kwao, Uganda.
Awali, Umony
alifanya mazungumzo na Simba SC ya Dar es Salaam pia na kufikia nao makubaliano,
lakini Wekundu hao wa Msimbazi kwa kitendo cha kuchelewa kumalizamna naye, sasa
‘wanaishia kunawa’.
Umony
alikuwa pia akiwaniwa na El Merreikh ya Sudan, ambayo nayo ilituma mwakilishi
wake kwenda kuzungumze naye Uganda wiki iliyopita.
Brian
amerejea nyumbani Uganda na kujiunga na KCC baada ya kumaliza mkataba wake, Becamex
Binh Duong F.C. ya Vietnam.
Mwaka 2009,
baada ya Simba kuzidiwa kete na SuperSport United ya Afrika Kusini, ikamsajili
Emmanuel Okwi aliyekuwa SC Villa wakati huo.
Umony
aliichezea Supersport United hadi 2010 alipohamia University of Pretoria ya Afrika
Kusini pia hadi mwaka 2011 alipohamia Portland Timbers ya Marekani kwa mkopo na
mwaka huu akatua Becamex Binh Duong F.C. Brian anang’ara katika Kombe la
Challenge, hadi sasa ana mabao matatu.