Kiungo wa Yanga, Nizar Khalfan akifumua shuti katikati ya mabeki wa Tusker katika mchezo wa leo wa kirafiki Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam |
Na Mahmoud Zubeiry
MABINGWA wa
Kenya, Tusker FC jioni hii wameiangusha Yanga SC bao 1-0 kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa kirafiki jioni hii.
Huo ulikuwa
mchezo maalum kwa Yanga kuwaaga mashabiki wake, kabla ya safari ya Uturuki
Jumamosi usiku kwenda kuweka kambi ya wiki mbili.
Wachezaji wa Tusker wakimpongeza mfungaji wa bao lao, Ismail Dunga kulia |
Hadi
mapumziko, Tusker walikuwa tayari mbele kwa bao hilo 1-0, lililowekwa kimiani
na kiungo Ismail Dunga kwa mkwaju wa penalti dakika ya 44.
Refa Charles
Oden Mbaga alitoa penalti hiyo baada ya kiungo wa Yanga, Nurdin Bakari
kumuangusha kwenye eneo la hatari, kiungo Khalid Aucho.
Yanga
walicheza vema katika kipindi hicho, lakini hawakufanikiwa kutengeneza nafasi
za kufunga na hilo lilitokana na mipango haba ya safu yake ya kiungo leo,
ikiongozwa na Kabange Twite na Nurdin Bakari.
Pamoja na
kocha Mholanzi Ernie Brandts kufanya mabadiliko kipindi cha pili, akiwaingiza Hamisi
Kiiza, Jery Tegete, Simon Msuva, Omega Seme na Nizar Khalfan kuchukuwa nafasi
za akina David Luhende, Said Bahanuzi, George Banda, Rehani Kibingu na Oscar
Joshua, lakini matokeo hayakubadilika.
Zaidi Yanga
iliongeza kasi ya mashambulizi kupitia kwa Msuva na Kiiza na hata Nizar
alipoingia, lakini kwa ujumla bahati haikuwa yao jioni ya leo.
Hii ni mechi
ya pili Brandts anafungwa kati ya mechi 10 alizoiongoza Yanga tangu aanze kazi
akirithi mikoba ya Mbelgiji, Tom Saintfiet, nyingine saba ameshinda na moja
ametoa sare.
Yanga SC;
Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’,
Ladislaus Mbogo, Nurdin Bakari, Rehani Kibingu, Kabange Twite, George Banda,
Said Bahanuzi na David Luhende.
Tusker FC;
George Opiyo, Luke Ochieng, Jeremiah Bright, Mark Odhiambo, Joseph Shikokoti, Khalid
Aucho, Edwin Manono, Justin Monda, Ismail Dunga, Jesse Were, Robert Omonuk,