• HABARI MPYA

        Wednesday, December 19, 2012

        TFF YATAFUTA NAMNA YA KUWAOKOA AKINA CANNAVARO, AGGREY


        Na Prince Akbar
        SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limepokea barua ya Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) ikieleza kuwafungia wachezaji kadhaa Wazanzibari wanaochezea klabu mbalimbali za timu za Tanzania Bara na timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars).
        Suala hilo limepelekwa kwa Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi ya TFF kwa hatua zaidi, hivyo kwa sasa Shirikisho litasubiri uamuzi wa kamati hiyo. Baadhi ya wachezaji hao ni nahodha msaidizi wa Taifa Stars, Aggrey Morris, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Nassoro Masoud Cholo, Mcha Khamis, Seif Abdallah na Selemani Kassim Selembe.
        Wachezaji hao, walifungiwa kwa kitendo cha kujiamualia kugawana fedha za zawadi ya ushindi wa tatu, dola za Kimarekani 10,000 katika Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge mwezi huu mjini Kampala, Uganda.

        • Blogger Comments
        • Facebook Comments
        Item Reviewed: TFF YATAFUTA NAMNA YA KUWAOKOA AKINA CANNAVARO, AGGREY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry