Amina Singo enzi za uhai wake |
Na Princess Asia
SHIRIKISHO
la Soka Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha aliyekuwa
mtangazaji wa habari za michezo katika kituo cha redio cha 100.5 Times FM,
Amina Singo kilichotokea usiku wa kuamkia jana.
Ofisa Habari
wa TFF, Boniface Wambura Mgoyo ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba msiba huo ni
mkubwa katika sekta ya habari na mpira wa miguu kwani kwa nyakati tofauti
kupitia taaluma ya uhandishi wa habari, Amina alifanya kazi na TFF, hivyo
mchango wake katika mpira wa miguu tutaukumbuka daima.
“Tutamkumbuka
kama mtangazaji wa habari za mpira wa miguu na michezo kwa ujumla. TFF tunatoa pole kwa familia za marehemu
Amina Singo, ndugu, jamaa na marafiki na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu
katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito,”alisema Wambura.
Mungu aiweke
roho ya marehemu Amina Singo mahali pema peponi. Amina