Na Dina Ismail
SHIRIKISHO
la Soka Tanzania (TFF) linaupongeza uongozi mpya wa Chama cha Mpira wa Miguu
Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) uliochaguliwa katika uchaguzi uliofanyika juzi
(Desemba 12 mwaka huu) hoteli ya Mbezi Garden.
Ushindi
aliopata Almasi Kasongo aliyechaguliwa kuwa Mwenyekiti pamoja na wajumbe
wengine wa Kamati ya Utendaji unaonesha jinsi ambavyo wajumbe wa Mkutano Mkuu
wa DRFA walivyo na imani kwao.
TFF inaahidi
kuendeleza ushirikiano wake kwa Kamati ya Utendaji ya DRFA ambayo hivi sasa ina
kinara mpya, na kwamba ina changamoto kubwa ya kuhakikisha inaendesha shughuli
za DRFA kwa kuzingatia katiba na kanuni.
Pia tunatoa
pongezi kwa Kamati ya Uchaguzi ya DRFA chini ya Juma Simba na Kamati ya
Uchaguzi ya TFF inayoongozwa na Deogratias Lyatto kwa kuhakikisha uchaguzi huo
unafanyika kwa utulivu na kwa kuzingatia katiba na Kanuni za Uchaguzi za
Wanachama wa TFF.
Safu mpya ya
uongozi wa DRFA inaundwa na Kasongo (Mwenyekiti), Meba Ramadhan (Makamu
Mwenyekiti), Msanifu Kondo (Katibu), Muhsin Said (Mwakilishi wa Mkutano Mkuu wa
TFF), Benny Kisaka (Mwakilishi wa Klabu), Ally Hobe (Mhazini) na wajumbe
Mohamed Shabani, Sunday Mwanahewa na Bakari Mapande.