• HABARI MPYA

        Saturday, December 22, 2012

        STARS YAJIPIMA NA MABINGWA WA AFRIKA KIBOKO YA AKINA YAYA TOURE NA DROGBA LEO TAIFA

        Taifa Stars

        Na Prince Akbar
        TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars leo inashuka kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kumenyana na mabingwa wa Afrika, Zambia ‘Chipolopolo’ katika mchezo wa kujipima nguvu kabla ya kwenda kutetea Kombe lao nchini Afrika Kusini mapema mwakani.
        Zambia imetua nchini na wachezaji 24, maofisa wengine wanane wakiwemo wa benchi la ufundi linaloongozwa na Kocha Mfaransa, Herve Renard aliyeipa timu hiyo ubingwa wa Afrika mwaka jana nchini Gabon.
        Wachezaji waliokuja na Zambia ni Chintu Kampamba, Chisamba Lungu, Christopher Katongo, Danny Munyau, Davy Kaumbwa, Derrick Mwansa, Evans Kangwa, Felix Katongo na Francis Kasonde.
        Wengine ni Given Singuluma, Hichani Himonde, Isaac Chansa, James Chamanga, Jimmy Chisenga, Jonas Sakuwaha, Joshua Titima, Kalililo Kakonje, Moses Phiri, Mukuka Mulenga, Rainford Kalaba, Rodrick Kabwe, Salulani Phiri, Shadrack Malambo na Stoppila Sunzu.
        Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager iko kambini jijini Dar es Salaam tangu Desemba 12 mwaka huu chini ya Kocha Mdenmark, Kim Poulsen kujiandaa kwa mechi hiyo.
        Viingilio katika mechi  ya leo vitakuwa Sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya bluu na kijani, Sh. 7,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, Sh. 10,000 kwa VIP C, Sh. 20,000 kwa VIP B wakati VIP A itakuwa Sh. 30,000.
        Tiketi zilianza kuuzwa tangu jana katika vituo vya Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Uwanja wa Uhuru, Mgahawa wa Steers ulioko Mtaa wa Ohio na Samora, Sokoni Kariakoo, kituo cha mafuta cha Ubungo OilCom na Dar Live Mbagala.
        Mara ya mwisho ilipojitupa dimbani Novemba 14, mwaka huu Stars iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Kenya, Harambee Stars kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza katika mchezo wa kirafiki, ambalo lililotiwa kimiani na beki Aggrey Morris katika dakika ya nne, baada ya kupanda kusaidia mashambulizi.
        Hii itakuwa mechi ya tisa kwa Stars mwaka huu, nane za awali, ikishinda mbili moja ya mashindano na moja ya kirafiki, kufungwa moja na sare tano.
        Iliifunga 2-1 Gabon katika mchezo wa kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia kabla ya kuifunga Kenya 1-0.

        REKODI YA STARS MWAKA HUU NA RATIBA YA MECHI ZIJAZO:
        Februari 23, 2012
        Tanzania 0 – 0 DRC (Kirafiki)
        Februari 29, 2012
        Tanzania 1 – 1 Msumbiji   (Kufuzu Mataifa ya Afrika)
        Mei 26, 2012
        Tanzania 0 – 0 Malawi
        Juni 2, 2012
        Ivory Coast 2 – 0 Tanzania (Kufuzu Kombe la Dunia)
        Juni 10, 2012
        Tanzania 2 – 1 Gambia      (Kufuzu Kombe la Dunia)
        Juni 17, 2012
        Msumbiji 1 – 1 Tanzania   (Tanzania ilitolewa kwa penalti kufuzu Mataifa ya Afrika)
        Agosti 15, 2012
        Botswana 3 – 3 Tanzania (Kirafiki)
        Novemba 14, 2012
        Tanzania 1-0 Kenya (Kirafiki)
        Desemba 22, 2012
        Tanzania Vs Zambia (Kirafiki)

        MECHI ZIJAZO
        Machi 22, 2013
        Tanzania Vs Morocco (Kufuzu Kombe la Dunia)
        Juni 7, 2013
        Morocco Vs Tanzania (Kufuzu Kombe la Dunia)
        Juni 14, 2013    
        Tanzania Vs Ivory Coast    (Kufuzu Kombe la Dunia)
        Septemba 6, 2013
        Gambia    Vs Tanzania (Kufuzu Kombe la Dunia)
        • Blogger Comments
        • Facebook Comments
        Item Reviewed: STARS YAJIPIMA NA MABINGWA WA AFRIKA KIBOKO YA AKINA YAYA TOURE NA DROGBA LEO TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry