Na Mahmoud Zubeiry,
Kampala
TANZANIA
Bara, Kilimanjaro Stars itacheza na Rwanda katika Robo Fainali ya Kombe la
Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge Jumatatu kwenye
Uwanja wa Lugogo kuanzia saa 8:00 mchana, wakati Zanzibar itacheza na Burundi
saa 10:00 jioni.
Robo Fainali
nyingine zitachezwa Jumanne Uwanja wa Mandela, Namboole, kati ya Kenya na Malawi
saa 10:00 jioni wakati wenyeji Uganda watacheza na Ethiopia saa 1:00 usiku.
Katika mechi
za leo, Bara iliilaza Burundi mabao 7-0 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja
wa Lugogo mjini hapa.
Matokeo hayo
yanaifanya Bara itimize pointi sita baada ya kucheza mechi tatu na sasa,
wakishinda mbili na kufungwa moja.
Burundi imemalizaa
kileleni mwa Kundi B, kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Sudan, bao pekee la
Chris Nduwarugira.
Rwanda imeifunga
Eritrea 2-0, mabao ya Tadi Etikiama na Tumaine Ntamuhanga, huku Malawi ikiilaza
Zanzibar 2-0.
Stars,
inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager leo ilionyesha kandanda safi na
kusisimua mashabiki wa Tanzania waliokuja kuoiunga mkono hapa, akiwemo Mbunge
wa Kondoa Kaskazini, Alhaj Juma Nkamia.
Iliwachukua
sekunde 48 tu Stars kupata bao la kwanza, kupitia kwa mshambuliaji wa Simba SC,
inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premum Lager pia, Mrisho Khlfan Ngassa
aliyewazidi ujanja mabeki wa Somalia.
Kabla
hawajakaa vizuri, Somalia walipachikwa bao la pili, dakika ya 23 lililofungwa
na Ngassa tena, aliyeunganisha kona nzuri ya Issa na Rashid.
John Bocco
‘Adebayor’ alifunga bao la tatu katika mchezo wa leo na la tatu kwake katika
mashindano haya dakika ya 26 akiunganisha kwa kichwa krosi ya Issa Rashid
kutoka wingi ya kushoto.
Bocco tena
aliwainua vitini mashabiki wa Tanzania kwa kufunga bao la nne kwa kichwa,
akiunganisha krosi ya Ngassa dakika ya 41.
Ngassa
alifunga bao la tatu katika mchezo wa leo dakika ya 44 na la tano kwa Stars
baada ya kuuwahi mpira uliotemwa na kipa Hussein Abdallah kufuatia shuti kali
la Salum Abubakar ‘Sure Boy Jr.’
Somalia
ilipata pigo dakika ya 30, baada ya kipa wake namba moja, Mohamed Abdullah
kuumia baada ya kugongana na Bocco na kutoka, nafasi yake ikichukuliwa na
Hussein Abdallah.
Kipindi cha
pili Stars walirejea na moto wao na tena na kufanikiwa kupata mabao mawili
zaidi yaliyotiwa kimiani na Ngassa yote dakika za 73 pasi ya Erasto Nyoni na 74
pasi ya Ramadhani Sinago ‘Messi’.
Kwa kufunga
mabao matano, Ngassa sasa ameingia kwenye mbio za kaiti cha dhahabu akikwa
anaongoza, akifuatiwa na Bocco ambaye ana manne hivi sasa.
Kocha wa
Stars, Mdenmark Kim Pouslen baada ya mchezo huo, alisema aliwapongeza vijana
wake kwamba wamejitahidi kucheza vizuri na akasifu pia hali nzuri ya Uwanja wa
Lugogo kuwa ilichangia ushindi huo.
Mbunge
Nkamia alisema kwamba amevutiwa na soka ya vijana leo na anaamini wana uwezo wa
kurejea na Kombe nyumbani. Nkamia aliwapongeza wadhamini wa Stars kwa kuchangia
mafanikio ya timu hiyo tangu waanze kuidhamini na akaomba Watanzania zaidi
wajitokeze mjini hapa kuisapiti timu hiyo.
Waandishi wa
Habari waliopo mjini hapa pia wamevutiwa mno na kiwango cha timu hiyo na kusema
wana wana imani itafika mbali.
Wallace
Karia, Mjume wa Kamati ya Utendaji ya TFF aliye hapa Uganda amesema
amefurahishwa na kiwango cha timu na anaamini itafika mbali.
Meneja wa
Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, wadhamini wa Kilimanjaro Stars, George
Kavishe ametuma salamu za pongezi kwa ushindi wa leo na mafanikio ya kutinga
Robo Fainali na kusema anatakia mafanikio zaidi timu hiyo.
Katika
mchezo wa leo, kikosi cha Stars kilikuwa; Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Issa
Rashid, Shomari Kapombe, Kevin Yondan/Ramadhani Singano, Shaaban Nditi, Mrisho
Ngassa, Salum Abubakar, John Bocco/Christopher Edrwad, Frank Domayo/Athumani
Iddi na Amri Kiemba.
Somalia;
Mohalim Abdullahi/Hussein Abdallah dk30, Ali Mohamed, Said Mahamud, Ali Dadir,
Sadaq Abdikadir, Mohamed Salah, Abdikarim Abubakar, Abdallah Mohamed/Hamza
Mukhtar, Ahmed Abdikadir Dahir/Muhad Hajji na Ali Ahmed Ali.
MSIMAMO
KUNDI A:
P W D L GF GA GD Pts
Uganda 3 3 0 0 6 0 6 9
Kenya 3 2 0 1 4 2 2 6
Ethiopia 3 1 0 2 2 3 -1 3
Sudan Kusini 3 0 0 3 0 7 -7 0
MSIMAMO
KUNDI B:
P W D L GF GA GD Pts
Burundi 3 3 0 0 7 1 6 9
Tanzania 3 2 0 1 9 1 9 6
Sudan 3 1 0 2 1 3 -2 3
Somalia 3 0 0 3 1 13 -12 0
MSIMAMO
KUNDI C:
P W D L GF GA GD Pts
Rwanda 3 2 0 1 5 2 3 6
Zanzibar 3 1 1 1 2 2 0 4
Malawi 3 2 0 1 5 4 1 6
Eritrea 3 0 1 2 2 5 -3 1
ROBO FAINALI
Desemba 3, 2012
Tanzania Vs Rwanda Saa
8:00 mchana Lugogo
Zanzibar Vs Burundi Saa
10:00 jioni Lugogo
Desemba 4, 2012
Kenya Vs
Malawi Saa 10:00 jioni Namboole
Uganda Vs
Ethiopia Saa 1:00 usiku Namboole