Ssentongo |
Na Mahmoud Zubeiry,
Kampala
MSHAMBULIAJI
wa Uganda, Robert Ssentongo amesema kwamba atakuwa tayari kujiunga na Simba SC
ya Dar es Salaam, wakiafikiana naye dau.
Ssentongo
anayeng’ara katika Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, amewahi
kuchezea Simba kwa muda tu katika Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, mwaka
juzi mjini Kigali, Rwanda.
Lakini baada
ya michuano hiyo, akatemwa na badala yake akasajiliwa kiungo Mganda mwenzake,
Patrick Ochan ambaye baada ya msimu mmoja aliuzwa TP Mazembe ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
“Mimi nipo
tayari Simba wakinitaka, wao wafike bei tu, ile ni timu kubwa na ninaamini
nikijiunga nayo nitapata mafanikio,”alisema.
Ssentongo
amewahi kucheza African Lyon ya Dar es Salaam na alipomaliza mkataba wake
akachezea Simba kwa muda kabla ya kurejea Uganda.
Awali
Ssentongo aliwahi kuchukua fedha za Simba, lakini hakuja kujiunga nayo hadi
alipokuja Lyon.