Kikosi cha Zanzibar, Selembe wa kwanza kushoto walioinama, kiboko ya Wakenya |
Na Mahmoud Zubeiry,
Kampala
KIUNGO wa
Zanzibar, Suleiman Kassim ‘Selembe‘ ndiye mchezaji ambaye anawatia hofu mno
Wakenya kuelekea mchezo wa leo wa Nusu Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika
Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge Uwanja wa Mandela, Namboole, mjini
hapa.
Mashabiki wa
soka wa Kenya waliopo hapa na baadhi ya Waandishi wa Habari kutoka nchini humo,
wamekuwa wakimzungumzia Selembe kama mchezaji hatari na aliyebeba hatima yao
leo.
“Selembe,
yule mchezaji yupo kama Fellaini
(Marouane) ni hatari sana yule, kwa kweli amebeba hatima yetu, tukiweza kumbana
yule, Zanzibar wala hawafurukuti,”alisema mmoja wa mashabiki wa Kenya juzi
mjini hapa, akimfananisha kiungo huyo na kiungo wa kimataifa wa Ubelgiji mwenye
asili ya Morocco, anayechezea Everton ya England.
Kenya na
Zanzibar zinamenyana katika Nusu Fainali ya kwanza kwenye Uwanja wa Mandela
leo, mchezo ambao utafuatiwa na mechi nyingine kati ya Uganda na Tanzania Bara.
Kenya
wanaonekana kuihofia mno Zanzibar kiasi cha kuthubutu kuwarejesha kambini
wachezaji wake wawili iliyowarudisha nyumbani kwa utovu wa nidhamu, Paul Were na
Kevin Omondi.
Baada ya
kuifunga 1-0 Sudan Kusini katika mchezo wa pili wa Kundi A, wachezaji hao
walikwenda kujirusha kwenye klabu ya usiku na kurejea kambini na wanawake,
jambo ambalo lilifanya asubuhi yake wapandishwe ndege wote kurejea Nairobi,
lakini kutokana na mchecheto wa mechi ya kesho, wamerejeshwa.
Kocha wa Harambee
Stars, James Nandwa aliliomba Shirikisho la Soka Kenya (FKF) liliwarejeshe
wachezaji hao kwa ajili ya Nusu Fainali.
Kocha wa Fisa
FC, Charles ‘Korea’ Omondi, ambaye amekuwa akifanya mazoezi na wachezaji hao
tangu warejeshwe nyumbani, amethibitisha wamebadilika kinidhamu na wako vizuri
kimchezo.
Were na
Omondi wapo kwa mkopo AFC Leopards na Gor Mahia kutoka timu inayoshiriki Ligi
ya Jimbo la Nairobi, Fisa FC.
Mara ya
kwanza na ya mwisho timu hizi kukutana katika hatua ya mtoano ilikuwa ni mwaka
1979 nchini Kenya, katika Nusu Fainali na wenyeji walishinda 2-0 Novemba 14
Uwanja wa Nyayo, Nairobi na mara zote zimekuwa zikikutana katika hatua ya
makundi.
Na mara ya
mwisho kabisa kukutana katika mashindano haya timu hizi ilikuwa ni mwaka 1996
nchini Sudan na Kenya ilishinda 1-0.
Kwa ujumla,
timu hizi zimekutana mara 11 tangu kuanzishwa rasmi kwa michuano ya Challenge
mwaka 1974 na Kenya imeshinda mechi saba, sare tatu na imefungwa moja. Kenya
imeifunga Zanzibar jumla ya mabao 17, wakati yenyewe imefungwa saba.
REKODI YA KENYA NA ZANZIBAR CHALLENGE
P W D L GF GA Pts
Kenya 11 7 3 1 17 7 24
Zanzibar 11 1 3 7 7 17 6
REKODI YA KENYA NA ZANZIBAR TANGU
1977:
Novemba 24, 1996; Sudan Kundi B
Kenya 1-0
Zanzibar
Novemba 27, 1995; Uganda Kundi A
Kenya 2-0
Zanzibar
Novemba 30, 1991; Kundi B Uganda
Kenya 3-2
Zanzibar
Desemba 6, 1989; Kundi B
Kenya
Zanzibar 0-0
Kenya B
Desemba 14, 1987; Kundi A Ethiopia
Kenya 0-0
Zanzibar
Desemba 6, 1984; Kundi B Uganda
Kenya 1-0
Zanzibar
Novemba 21, 1982; Kundi B
Uganda
Kenya 2-2
Zanzibar
Novemba 17, 1981; Kundi A Tanzania
Kenya 2-1
Zanzibar
Novemba 22, 1980; Kundi B Sudan
Kenya 1-2
Zanzibar
Novemba 14, 1979; Nusu Fainali Kenya
Kenya 2-0
Zanzibar
Desemba 2, 1977; Kundi A Somalia
Kenya 3-0
Zanzibar