Bocco akiwawajibisha mabeki wa Rwanda juana |
Na Mahmoud Zubeiry, Kampala
KAMA si refa
kukataa bao lake safi tu alilofunga katika mechi ya Kundi B dhidi ya Burundi,
leo Bocco angekuwa kileleni kwenye msimamo wa wafungaji wa mabao katika Kombe
la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge kwa mabao sita,
lakini kufanyiwa dhuluma hiyo ana mabao matano.
Hata hivyo,
jambo moja tu ameonyesha Bocco mjini hapa, yeye ni mfungaji wa uhakika
anapocheza kwenye mazingira mazuri pasipo kuzomewa zomewa na mashabiki anapokosea
kidogo kibinadamu.
Hiyo inatokana
na Bocco kufunga katika mechi aliyocheza kuanzia hatua ya makundi, dhidi ya Sudan
mabao mawili, Burundi moja lililokataliwa, Somalia mawili na jana mojas dhidi
ya Rwanda.
Bocco sasa
ina idadi sawa ya mabao na Mrisho Ngassa wa Tanzania Bara pia, ambaye yeye
alifunga mabao yote katika mechi moja dhidi ya vibonde Somalia.
Bocco na
Ngassa wanafuatiwa kwa mbali na Brian Umony wa Uganda mwenye mabao matatu, sawa
na Warundi wawili, Suleiman Ndikumana na Christopher Nduwarugira katika mbio za
kiatu cha dhahabu cha mashindano haya.
Khamis Mcha ‘Vialli’
wa Zanzibar, David Ochieng, Clifton Miheso wote wa Kenya na Dadi Birori au
Taddy Etikiama wa Rwanda, wote wana mabao mawili kila mmoja.
WAFUNGAJI CECAFA TUSKER CHALLENGE
2012
John Bocco Tanzania 5
Mrisho
Ngassa Tanzania 5
Brian Umony Uganda 3
Suleiman
Ndikumana Burundi 3 (1 penalti)
Chris
Nduwarugira Burundi 3
Khamis Mcha Zanzibar 2
David
Ochieng Kenya 2
Clifton
Miheso Kenya 2
Dadi Birori Rwanda 2