Ngassa |
WAKATI Kombe
la Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge,
linafikia tamati leo mjini Kampala, Uganda ushindani mkubwa umeibuka katika
kinyang’anyiro cha ufungaji bora wa mashindano hayo yaliyoanza Novemba 24,
mwaka huu mjini hapa.
Washambuliaji
wa Tanzania Bara, John Raphael Bocco na Mrisho Khalfan Ngassa hadi sasa
waongoza, kila mmoja akiwa na mabao matano, wakifuatiwa na Robert Ssentongo wa
Uganda, mwenye mabao manne.
Uganda leo itamenyana
na Kenya katika fainali na Ssentongo atakuwa na nafasi nyingine ya kufunga,
wakati Bara itamenyana na Zanzibar kusaka nafasi ya tatu na Ngassa na Bocco pia
watakuwa na nafasi ya kuongeza mabao pia.
Lakini pia
watatu hao wote wanaweza kuikosa tuzo hiyo, iwapo wachezaji wengine wenye mabao
matatu watafunga idadi kubwa ya mabao katika mechi za leo na wao wakatoka kapa.
Hao ni Brian
Umony wa Uganda mwenye mabao matatu, sawa Khamis Mcha ‘Vialli’ wa Zanzibar. Suleiman
Ndikumana na Chris Nduwarugira wa Burundi, nao pia wana mabao matatu kila
mmoja, lakini timu yao imekwishatolewa.
Wachezaji
wenye mabao mawili kila mmoja ni Geoffrey Kizito wa Uganda, David Ochieng, Mike
Barasa, Clifton Miheso wa Kenya na Dadi Birori wa Rwanda, ambao timu yao
imekwishatolewa.
WAFUNGAJI CECAFA TUSKER CHALLENGE
2012
John Bocco Tanzania 5
Mrisho
Ngassa Tanzania 5
Robert
Ssentongo Uganda 4
Brian Umony Uganda 3
Khamis Mcha Zanzibar 3
Suleiman
Ndikumana Burundi 3 (1 penalti)
Chris
Nduwarugira Burundi 3
Geoffrey
Kizito Uganda 2
David
Ochieng Kenya 2
Clifton
Miheso Kenya 2
Dadi Birori Rwanda 2
Mike Barasa Kenya 2