// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MWINYI KAZIMOTO AWAPONEA RWANDA, KAZI IPO KESHO LUGOGO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MWINYI KAZIMOTO AWAPONEA RWANDA, KAZI IPO KESHO LUGOGO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, December 02, 2012

    MWINYI KAZIMOTO AWAPONEA RWANDA, KAZI IPO KESHO LUGOGO

    Kazimoto mazoezini leo
    Na Mwandishi wetu, Kampala
    KIUNGO wa timu ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars, Mwinyi Kazimoto amepona na leo amefanya mazoezi na wenzake Kim, Uwanja wa Chuo Kikuu cha Kyambogo mjini hapa tayari kucheza mechi ya Robo Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge dhidi ya Rwanda kesho.
    Kocha Mkuu wa Stars, Mdenmark, Kim Poulsen amefurahia kupona kwa kiungo huyo wa Simba SC na anaamini itakuwa moja ya silaha zake katika mchezo wa kesho dhidi ya Rwanda Uwanja wa Lugogo, ambao utaanza saa 8:00 mchana.
    Kazimoto aliumia katika mechi dhidi ya Burundi na akakosa mechi ya mwisho ya Kundi B dhidi ya Somalia jana, lakini kesho atakuwa kazini tena.
     “Rwanda ina timu nzuri na tunaiheshimu sana lakini tuko tayari kupambana nao katika mechi ya kesho na ninaamini vijana wataendelea kufunga mabao kama ilivyofanyika katika mechi dhidi ya Somalia,” alisema.
    Kocha huyo alisema wachezaji wote wako katika hali nzuri na wana ari ya kushinda mechi hii ili watinge katika hatua ya nusu fainali.
    “Vijana wana morali na wamejiandaa vizuri na mechi hii ya kesho na tuna imani watatupa raha tena kama Jumamosi.
    Katika hatua nyingine, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kaishe ambaye Bia ya kampuni yake  inaidhamini Kilimanjaro Stars, alitoa pongezi kwa Stars kwa kutinga hatua ya robo fainali.
    “Tumekuwa tukifuatilia mashindano haya kwa njia ya runinga na kwa kweli yameleta hamasa kubwa sana hasa mchezo wa Jumamosi tulipoifunga Somaliake kwa vya 7-0,” alisema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.
    Kavishe alisema Stars ina uwezo mkubwa wa kutinga fainali na kurejea nyumbani na kombe hili la Cecafa.
     “Watanzania wote lazima wawe na imani na waiombee dua njema timu yetu ili ishinde…sisi tukiwa wadhamini tutaendelea kuipa nguvu timu wao watuletee kombe tu,” alisema.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: MWINYI KAZIMOTO AWAPONEA RWANDA, KAZI IPO KESHO LUGOGO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top