Somoe Ng'itu |
Na Mwandishi
Wetu, Kampala
MWANDISHI
mwandamizi wa michezo wa gazeti la NIPASHE, Somoe Ng'itu, juzi alichaguliwa
kuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji (Wanawake) ya Chama cha Waandishi wa Habari
za Michezo wa Afrika Mashariki na Kati (ECASJA).
Somoe
alishinda nafasi hiyo baada ya kupata kura nne kati ya saba ambapo alimshinda
mwandishi, Lydia Namakula wa New Vision ya Uganda huku Katibu Mkuu wa zamani wa
TASWA, Abdul Mohamed alichaguliwa kuwa Mweka Hazina.
Katika
uchaguzi huo uliowahusisha waandishi mbalimbali wa habari za michezo kutoka
katika ukanda wa CECAFA ambao wako jijini hapa wakiripoti mashindano ya Kombe
la Chalenji yanayoendelea jijini hapa, Mark Namanya, ambaye ni Mwenyekiti wa
Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo wa Uganda (USPA), alichaguliwa kuwa
mwenyekiti.
Nafasi ya
Makamu Mwenyekiti ilichukuliwa na Bonnie Mugabe wa Rwanda, Mike Okinyi (Katibu
Mkuu).
Wajumbe
wengine waliochaguliwa katika chama hicho ambapo watakaa kwa muda wa mwaka
mmoja madarakani ni pamoja na Desire Hatugimana (Burundi), Patrick Kanyamozi
(Uganda).
Moja ya
malengo ya chama hicho ambacho kilianzishwa mwaka 1982 lakini kilikufa ni
kuendeleza taaluma ya waandishi wa michezo katika ukanda wa CECAFA na kukuza
michezo yote.