Ridhiwani, mtu wa watu |
Na Amir Mhando
MAANDALIZI
ya Mkutano Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA)
yanaenda vizuri na wajumbe wanatarajiwa kufika Bagamoyo kesho (Desemba 28, 2012)
mchana kwenye hoteli ya Kiromo View Resort watakapolala na kufanyia mkutano.
Ijumaa hiyo
washiriki watatembelea maeneo mbalimbali ya kihistoria Bagamoyo na jioni
kutakuwa na mechi ya kirafiki kati ya timu ya soka ya TASWA FC na Bagamoyo
Veterani itakayofanyika Uwanja wa Mwanakalenge na usiku wajumbe watakuwa na
chakula cha pamoja na kubadilishana mawazo kuhusiana na masuala mbalimbali
yahusiyo michezo na taaluma ya habari.
Mkutano Mkuu
utafunguliwa Jumamosi Desemba 29, saa tatu asubuhi na mgeni rasmi atakuwa
Mwenyekiti wa Kamati ya Kusaidia timu za Taifa za Vijana, Ridhiwani
Kikwete.TASWA imechukua jukumu la kumualika kutokana na kuwa mdau mkubwa na
rafiki wa chama chetu.
Mkutano
utafungwa jioni ya siku hiyo na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Assah
Mwambene ambaye hiyo pia itakuwa nafasi nzuri kwake kuweza kuzungumza na wana
habari kuhusiana na masuala mbalimbali ya kitaaluma.
Katika
mkutano huo wanachama wa TASWA watapata fursa ya kupokea na kujadili Ripoti ya
Utendaji ya chama, Mapato na Matumizi, maendeleo ya chama na masuala mbalimbali
yanayohusu waandishi wa habari za michezo na maendeleo ya michezo kwa ujumla
Pia kutakuwa
na semina maalum itakayoendeshwa kwa washiriki wa mkutano huo, ili wawe na
uelewa kuhusiana na ajenda ya kuinua kipato kwa wanachama ambayo nayo
itajadiliwa kwenye mkutano huo.
Kamati ya
Utendaji ya TASWA imekubaliana iwasaidie wanachama wake waweze kujitegemea kwa
kuanzisha Chama cha Akiba na Mikopo (SACCO’S), lakini imeamua kwanza iwaite
wataalamu wa vyama vya ushirika watoe elimu juu ya jambo hilo na kukishakuwa na
uelewa wa kutosha suala hilo litakuwa kama ajenda kamili ya kuanzisha chama
hicho kwenye mkutano wetu.
(Mwandishi wa habari
hizi ni Katibu Mkuu wa TASWA)