|
Bondia Francis Miyeyusho akiwa amebebwa na mashabiki wake kwenye ukumbi wa PTA, Saba Saba, Temeke mjini Dar es Salaam usiku huu baada ya kutetea mataji yake ya kimataifa kwa kumpiga Nassib Ramadhan kwa Technical Knockout (TKO) raundi ya 10. |
Na Mahmoud Zubeiry
BONDIA Francis
Miyeyusho ‘Chichi Mawe’ amefanikiwa kutetea taji lake la WBF uzito wa Bantam,
baada ya kumpiga Nassib Ramadhan kwa Techinical Knockout (TKO) raundi ya 10 kwenye
ukumbi wa PTA, Saba Saba, Temeke mjini Dar es Salaam usiku huu.
Nassib alionekana
kuishiwa pumzi tangu raundi ya nane, lakini alijikongoja kutaka kumaliza raundi
12 za pambano hilo, ila kwa bahati mbaya, safari ikaishia raundi ya 10.
Hata hivyo,
Nassib bondia kutoka Mabibo, Dar es Salaam, alilianza vizuri pambano hilo
akimsukumia mpinzani wake makonde mazito yaliyoonekana kumyumbisha.
Naasib
aliendelea kutawala pambano hadi raundi ya sita, ila baada ya hapo, mwelekeo wa
pambano ulianza kubadilika taratibu, Chichi, Mtoto wa Kinondoni akianza kumuadhibu
mpinzani wake kwa makonde yake yaliyoshiba uzito.
Nassib alijitahidi
mara moja moja kujibu, lakini zaidi alitumia ujanja wa kumkumbatia Chichi ili
kumpunguza kasi.
Hata hivyo,
Nassib hakushindwa kwa kupigwa ngumi, bali aliishiwa pumzi jambo ambalo
linaashiria kijana huyo ni bondia imara na anaweza kuwa mpinzani wa kweli wa
Chichi Mawe.
Kwa ujumla
lilikuwa pambano zuri ambalo kwa muda mrefu halijapatikana katika ardhi ya
Tanzania- mabondia walikuwa wakipigana, hakukuwa na ujanja ujanja. Wote ni
mafundi na mamia waliohudhuria pambano hilo, waliburudika kwa mchezo mzuri.
Katika mapambano
ya awali, Deo Samuel alitoka sare na Freddy Sayuni, Mohamed Matumla alimpiga
kwa Knockout (KO) raundi ya pili Deo Miyeyusho, Fadhil Majiha alimpiga kwa
pointi Juma Fundi na Ibrahim Classic alimpiga kwa pointi Said Mbugi.
Mgeni rasmi,
Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara alimvalisha mkanda
wa ubingwa Miyeyusho baada ya pambano hilo, lililohudhuriwa pia na Makamu
Mwenyekiti wa Simba SC, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’.
|
Mbwana Matumla katikati akiwa George Njavike kulia na King Kiboya kushoto |
|
Hassan matumla na mkewe |
|
Promota Mohamed Bawaziri akiwa Mh, Dk Fenlela |
|
Jamaa alizima mapemaaa, hajaangalia pambano sasa sijui atasimulia nini kitaa |
|
Ibrahim Classic kushoto akimuadhibu Said Mbugi |
|
Bondia mstaafu, Koba Kimanga akizungumza na Thomas Mashali |
|
Msafiri Mgoyi wa TFF akiwa na Yassin Ustadh |
|
Mabondia wastaafu, Emmanuel Mlundwa na Habib Kinyogoli |
|
Mohamed Matumla akimuadhibu Deo Miyeyusho |
|
Mohamed Matumla akimuadhibu Deo Miyeyusho |
|
Mohamed Matumla akiwa amebebwa juu baada ya kushinda kwa KO raundi ya pili |
|
Juma Fundi kulia akimtupia konde Fadhil Majiha |
|
Jaji akifuatilia kwa makini pambano |
|
Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto kulia akiwa na Dk Fenella meza kuu |
|
Kutoka kulia Makamu Mwenyekiti wa Simba SC, Geoffrey Nyange 'Kaburu', Mzee Matumla na Benny Kisaka |
|
Nassib akimtupia konde Francis Miyeyusho |
|
Nassib na Miyeyusho |
|
Nassib na Miyeyusho |
|
Nassib na Miyeyusho |
|
Miyeyusho akimsukumi kitu Nassib |
|
Nassib na Miyeyusho |
|
Konde la Miyeyusho limetua kwenye uso wa Nassib |
|
Nassib na Miyeyusho |
|
Nassib na Miyeyusho |
|
Full maufundi, Nassib na Miyeyusho |
|
Nassib na Miyeyusho |
|
Nassib na Miyeyusho |
|
King Miyeysho ukipenda muite Chichi Mawe |
|
Nassib akiwa amebebwa kutolewa ulingoni |
|
Dk Fenell akimvalisha mkanda Miyeyusho, kushoto ni Mohamed Bawaziri |