Atudo |
Na Mahmoud Zubeiry
BEKI
Joackins Atudo na kiungo Humphrey Mieno wamebaki nyumbani kwao Nairobi, Kenya
na watajiunga tena na kikosi cha Azam FC, baada ya sikukuu za Krisimasi na
mwaka mpya.
Wawili hao,
walikuwepo kwenye kikosi cha Azam kilichotwaa Kombe la Hisani, linaloandaliwa
na FECOFA, Shirikisho la Soka la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC),
Jumamosi iliyopita, wakiwachapa wenyeji Dragons FC kwa penalti 4-2 kufuatia
sare ya 2-2 ndani ya dakika 90.
Ikiwa njiani
kurejea Dar es Salaam, Meino na Autdo waliteremka Nairobi wakati mabingwa hao
wa Kombe la Hisani wakiwasili Tanzania usiku wa saa 7:00 jana.
Katibu wa
Azam, Nassor Idrisa amesema wachezaji wengine pia watapewa mapumziko ya siku
mbili kwa ajili ya sikukuu ya Krisimasi na baada ya hapo watakutana kujiandaa
kwa safari ya Zanzibar kwenda kutetea Kombe lao la Mapinduzi.
Azam Jumamosi
ilitwaa ubingwa wa Kombe la Hisani baada ya kuwafunga wenyeji, Dragons FC kwa
penalti 4-2, kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 90 kwenye Uwanja wa Martyrs
mjini Kinshasa.
Azam
walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 12 kabla ya Dragons kusawazisha
dakika ya 75 na katika mikwaju ya penalti, kipa Mwadini Ally alicheza mikwaju
miwili ya Dragons, wakati Gaudence Mwaikimba, Himid Mao, Joackins Atudo na
Samih Hajji Nuhu walifunga penalti za Azam.
Azam iliingia
fainali, baada ya kufanikiwa kuitoa kwa mikwaju ya penalti 5-4 Shark FC ya DRC
Ijumaa, kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 90 kwenye Uwanja wa Martyrs.
Kikosi cha
Azam kilichoshiriki mashindano hayo ni Kipre Tchetche, Seif Abdallah, Kipre
Balou, Zahor Pazi, Jackson Wandwi, Malika Ndeule, Uhuru Suleiman, Omar Mtaki,
Jabir Aziz, Ibrahim Mwaipopo, Gaudence Mwaikimba, Abdi Kassim, Luckson Kakolaki,
Samih Hajji Nuhu, Mwadini Ally, Himid Mao, David Mwantika, Waziri Salum, Humphrey
Mieno na Joackins Atudo.
Katika
mashindano hayo, Gaudence Mwaikimba aliibuka mfungaji bora kwa mabao yake
matatu, ukiachilia mbali mawili ya penalti. Mchezaji mwingine wa kigeni wa
Azam, Brian Umony wa Uganda, atajiunga na timu hiyo baada ya sikukuu pia.