Waziri Salum |
Na Prince Akbar
VIUNGO wa
Zanzibar, Waziri Salum na Abdulhalim Humud hawatacheza michuano ya Kombe la
Mapinduzi, inayoanza wiki ijayo visiwani Zanzibar kutokana na kuwa bado
majeruhi.
Meneja
Msaidizi wa Azam, Jemadari Said Kazumari aliiambia BIN ZUBEIRY jana kwamba,
wawili hao hadi jana walikuwa hawajaripoti mazoezini, hivyo uwezekano wao wa
kucheza michuano hiyo ni mdogo.
Azam ambao
ndio mabingwa watetezi wa taji hilo na mabingwa wa Kombe la Hisani la DRC, walianza
mazoezi jana kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar
es Salaam, baada ya mapumziko mafupi ya sikukuu ya Krisimasi.
Katika
maozezi hayo, wachezaji wengine watatu walikosekana, beki Joackins Atudo,
kiungo Humphrey Mieno wote wa Wakenya na mshambuliaji Brian Umony wa Uganda kwa
sababu bado wana udhuru hadi baada ya sikukuu ya Krisimasi.
Azam ilitua
Dar es Salaam Jumatatu usiku wiki hii, ikitokea Kinshasa, Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ilikotwaa Kombe la Hisani, linaloandaliwa na
FECOFA, Shirikisho la Soka la DRC.
Azam
walitwaa taji hilo Jumamosi iliyopita, baada ya kuwachapa wenyeji, Dragons FC
kwa penalti 4-2 kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 90.
Azam iliingia
fainali, baada ya kufanikiwa kuitoa kwa mikwaju ya penalti 5-4 Shark FC ya DRC
Ijumaa, kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 90 kwenye Uwanja wa Martyrs.
Kikosi cha
Azam kilichoshiriki mashindano hayo ni Kipre Tchetche, Seif Abdallah, Kipre
Balou, Zahor Pazi, Jackson Wandwi, Malika Ndeule, Uhuru Suleiman, Omar Mtaki,
Jabir Aziz, Ibrahim Mwaipopo, Gaudence Mwaikimba, Abdi Kassim, Luckson Kakolaki,
Samih Hajji Nuhu, Mwadini Ally, Himid Mao, David Mwantika, Waziri Salum, Humphrey
Mieno na Joackins Atudo.
Katika
mashindano hayo, Gaudence Mwaikimba aliibuka mfungaji bora kwa mabao yake
matatu, ukiachilia mbali mawili ya penalti. Mchezaji mwingine wa kigeni wa
Azam, Brian Umony wa Uganda, atajiunga na timu hiyo baada ya sikukuu pia.
Azam
wamepangwa Kundi B, katika Kombe la Mapinduzi pamoja na Mtibwa Sugar ya Morogoro,
Coastal Union ya Tanga na Miembeni ya Unguja.
Kundi A lina
timu za Simba SC, Tusker FC ya Kenya, Bandari ya Unguja na Jamhuri ya Pemba.
Michuano ya Kombe
la Mapinduzi, ambayo ni maalum kwa ajili ya kuherehekea Mapinduzi matukufu ya
Zanzaibar, inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Januari 2, hadi kilele cha miaka 49
ya Mapinduzi ya Zanzibar, Januari 12, mwakani, huku ikishirikisha timu kutoka
ndani na nje ya Tanzania.