Liewig |
Na Mahmoud Zubeiry
KOCHA wa
zamani wa Akademi ya Paris Saint Germain (PSG) ya Ufaransa, ASEC Mimosas ya
Ivory Coast na Club Africain ya Tunisia, Patrick Liewig ndiye atakayerithi
mikoba ya Mserbia, Profesa Milovan Cirkovick katika klabu ya Simba.
Katibu wa
Simba SC, Evodius Mtawala ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, Liewig
atatua nchini baada ya Krisimasi kuja kuanza kazi.
“Atakuja
nchini baada ya krisimasi, kila kitu safi akifika anasaini mkataba na kuanza
kazi,”alisema Mtawala.
Liewig ana Stashahada
ya Juu ya ukocha na Shahada ya tatu ya ualimu wa soka ya vijana aliyotunukiwa
na Mkurugenzi wa Ufundi wa Ufaransa, Gerard Houiller na amehudhuria pia kozi za
ufundishaji mazoezi ya viungo Juni mwaka 1999 katika Chuo Kikuu cha Dijon.
Kwa upande wa
uzoefu, Liewig alifanya kazi PSG kuanzia mwaka 1989 hadi 1999 kama Kocha Mkuu
wa akademi na kuna wakati alikuwa akishirikishwa pia katika programu za timu A,
ingawa majukumu yake zaidi yalikuwa ni kwa Under 20, Under 18 aliowawezesha
kutwaa Kombe la French Junior Gambardella na Under 16.
Kuanzia mwaka
1989 hadi 1990: alikuwa Meneja Mkuu wa Tomislav
IVIC, 1990 hadi 1991 alikuwa Msaidizi wa Henri Michel, 1991 hadi 1994 alikuwa
Msaidizi wa Artur Jorge, 1994 hadi 1996 alikuwa Msaidizi wa Luis Fernandez, 1996
hadi 1998: alikuwa Msaidizi wa Ricardo Gomez, 1998 hadi 1999 alikuwa Msaidizi wa
Alain Giresse.
Liewig pia
alifundisha Al Wahda FC ya Abu Dhabi kuanzia 1999 hadi 2001, ambayo aliipa
ubingwa wa Ligi Kuu ya nchi hiyo na Kombe la Ligi.
Januari mwaka
2003 alikuwa Msimamizi wa Chama cha Soka UAE katika fainali za Afrika za U20 nchini
Burkina Faso.
Kuanzia mwaka
2004 hadi 2009 alikuwa Kocha wa ASEC Mimosas ya Ivory Coast aliyoipa mataji
matatu ya Ligi Kuu ya nchini humo mfululizo, 2004, 2005 na 2006, Super Cup ya
nchini humo 2005, 2007, 2008 na 2009 na akaiwezesha kufuzu hatua ya makundi ya
Ligi ya Mabingwa mara tatu, mara moja akiifikisha Nusu Fainali.
Amekuwa
Kocha bora wa Ivory Coast miaka mitatu mfululizo, 2004, 2005 na 2006 na tangu Septemba
mwaka jana hadi Juni mwaka huu, alikuwa kocha wa Club Africain ya Tunisia