Katongo |
Na Prince Akbar
KOCHA Mkuu
wa timu ya Zambia, Chipolopolo, ambayo ni mabingwa wa Afrika, Herve Renard
ametaja kikosi cha wachezaji 24 kitakachoikabili Taifa Stars kwenye mechi ya
kirafiki itakayochezwa Desemba 22 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu
wa Chama cha Soka Zambia (FAZ), wachezaji hao ni Chintu Kampamba, Chisamba
Lungu, Christopher Katongo, Danny Munyau, Davy Kaumbwa, Derrick Mwansa, Evans
Kangwa, Felix Katongo na Francis Kasonde.
Wengine ni
Given Singuluma, Hichani Himonde, Isaac Chansa, James Chamanga, Jimmy Chisenga,
Jonas Sakuwaha, Joshua Titima, Kalililo Kakonje, Moses Phiri, Mukuka Mulenga,
Rainford Kalaba, Rodrick Kabwe, Salulani Phiri, Shadrack Malambo na Stoppila
Sunzu.