ZH Poppe aifafanua mambo |
Na Mahmoud Zubeiry
MWENYEKITI
wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema kwamba, wamemtumia
tiketi kipa namba moja wa Uganda, Abbel Dhaira leo na atatua Dar es Salaam kesjokutwa
kwa ajili ya kusaini mkataba wa kuanza kuitumikia klabu hiyo.
Akizungumza
na BIN
ZUBEIRY leo, Kapteni huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania
(JWTZ) aliyepigana vita dhidi ya Uganda, alisema kwamba awali, Dhaira ilikuwa
atue leo, lakini kutokana na kukosa ndege sasa atatua keshokutwa.
Kuhusu suala
la mshambuliaji Brian Umony pia wa Uganda, Hans Poppe alisema; “Kuna ujgumu
kidogo, huyo tunaweza kumkosa,”alisema.
Kwa upande
wake, Dhaira amekwishasema kimsingi yeye yuko tayari kujiunga na Simba kwa kuwa
ni klabu kubwa Afrika na inacheza Ligi ya Mabingwa Afrika na angependa kuungana
na Mganda mwenzake, Emmanuel Okwi huko.
Tayari Simba
SC imefikia makubaliano na kipa huyo namba moja wa Uganda, aliyemaliza mkataba wake
na klabu ya I.B.V FC ya Iceland na amekubali kusaini mkataba wa miaka miwili
kwa dau ambalo halijafahamika.
Dhaira
alisema kwamba amefikia makubaliano na Simba kusaini mkataba wa miaka miwili
kuja kuanza maisha mapya Dear es Salaam.
Dhaira
ambaye aliibukia Express ya hapa mwaka 2006 kabla ya 2008 kuhamia U.R.A. pia ya
hapa, ambayo aliichezea hadi 2010 alipohamia Ulaya atatua Dar es Salaam
Jumatatu kumaliza kila kitu Simba.
Ikimpata
Dhaira, Simba SC itakuwa imepata kipa wa uhakika wa kusaidiana na kipa wake wa
kwanza, Juma Kaseja ambaye amekuwa akisotoshwa peke yake bila kupumzika. Na
hiyo inafuatia makipa wengine, Wilbert Mweta na Hamadi Waziri kushindwa
kuonyesha uwezo wa kumsaidia Kaseja.
Katika mechi
za mwishoni za mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, Kaseja
alionekana kuchoka na kudaka chini ya kiwango chake, jambo ambalo lilisababisha
mashabiki wenye ‘akili mbovu’ wamfanyie fujo baada ya kufungwa mabao mawili
katika mechi dhidi ya Mtibwa Sugar, Simba ikilala 2-0.
Kwa sababu
hiyo, Kaseja alikasirika na kujiengua kwenye kikosi cha timu hiyo akisema
hataki tena kuchezea Simba.
Lakini
pamoja na matatizo hayo, Kaseja aliitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ambako
ameendelea kufanya vizuri na kuonyesha yeye ni Tanzania One wa ukweli.